2023
Kuwatunza Wale Walio na Mahitaji
Septemba 2023


“Kuwatunza Wale Walio na Mahitaji,” Liahona, Machi 2023.

Misingi ya Injili

Kuwatunza Wale Walio na Mahitaji

Picha
Yesu akiwaponya watu

Aliponya Magonjwa Mengi ya Kila Aina, na J. Kirk Richards, isinakiliwe

Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunafuata mafundisho ya Bwana ya kuwajali wale wenye uhitaji. Tunawajali wengine kwa kuwatumikia, kuwasaidia wajitegemee, na kushiriki kile tulichonacho.

Mfano wa Yesu Kristo

Yesu Kristo aliwapenda, aliwafariji, na kuwaombea wale walio karibu Naye. Yeye “alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema ” (Matendo ya Mitume 10:38). Tunaweza kufuata mfano Wake kwa kuwapenda, kuwatumikia, na kuwaombea wale walio karibu nasi. Sisi daima tunaweza kutafuta njia za kuwasaidia wengine.

Picha
watu wawili wakitembea

Uhudumiaji

Neno uhudumiaji limetumika katika maandiko na katika Kanisa la Bwana kuelezea: jinsi tunavyoweza kujaliana mmoja na mwingine. Wenye ukuhani wanapangiwa kama akina kaka wahudumiaji kwa kila mtu au familia katika kata au tawi. Akina dada wahudumiaji wanapangiwa kwa kila mwanamke mtu mzima. Akina kaka na akina dada wahudumiaji wanahakikisha kwamba waumini wote wa Kanisa wanakumbukwa na kutunzwa.

Picha
watu wakipanda miche

Kuwasaidia Wengine Kuwa Wenye Kujitegemea

Tunaweza kuwasaidia wanafamilia na marafiki kuwa wenye kujitegemea kwa kuwahimiza wao kupata masuluhisho ya muda mrefu kwenye shida zao. Tunaweza kisha kuwasaidia wafanyie kazi malengo yao. Tafuta maelezo zaidi kuhusu kujitegemea katika Liahona ya Agosti 2023 Makala ya Misingi ya Injili.

Kuwahudumia Wengine

Kuna njia nyingi tunazoweza kuwatumikia wale walio karibu nasi na kuwasaidia kukidhi mahitaji yao kimwili, kiroho, na kihisia. Kujifunza kuhusu wengine kunaweza kutusaidia kujua jinsi tunavyoweza kuwatumikia vyema. Tunaweza pia kusali kwa ajili ya mwongozo ili kujua kile tunachoweza kufanya ili kusaidia.

Picha
watu wakikusanya matunda

Kushiriki Kile Tulichonacho

Tunaweza kuwasaidia wengine kwa kushiriki kile ambacho Mungu ametubariki nacho. Kwa mfano, tunaweza kutoa matoleo ya mfungo au kuchangia mfuko wa Msaada wa Kibinadamu wa Kanisa. Tunaweza pia kutumikia katika jamii yetu na miito yetu ya Kanisa.

Wajibu wa Viongozi wa Kanisa

Askofu husimamia kuwatunza wale walio na uhitaji katika kata. Anaweza kutumia hela kutoka kwenye matoleo ya mfungo kuwasaidia waumini walio na mahitaji. Viongozi wengine, ikijumuisha washauri wake na urais wa Muungano wa Usaidizi na urais wa akidi ya wazee, wanawasaidia waumini kupata nyenzo wanazoweza kutumia kukidhi mahitaji yao.

Juhudi za Msaada wa Kibinadamu wa Kanisa

Kanisa husaidia watu kote ulimwenguni katika dharura, miradi ya jamii, na mipango mingine kama vile maji safi na chanjo. Ili kujifunza zaidi, ona Dallin H. Oaks, “Kuwasaidia Masikini na Walio na Dhiki,” Liahona, Mei 2022, 6–8.