2023
Je, Ungependa Kujua Zaidi?”
Septemba 2023


Je, Ungependa Kujua Zaidi?,” Liahona, Septemba 2023.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Je, Ungependa Kujua Zaidi?”

Mojawapo wa wanahema wenzangu alikuwa tofauti na askari wengine, kwa hiyo nilimuuliza kwa nini yuko hivyo.

Picha
mwanamume akibatizwa ziwani

Mwandishi alibatizwa na Thomas Salisbury katika Ziwa Sông Bé, Vietnamu.

Picha kwa hisani ya mwandishi

Nilijiandikisha katika Jeshi la Marekani kwa muda wa miaka mitatu na kuwasili Vietnamu Kusini katika siku ya kutimiza miaka 20 ya kuzaliwa kwangu. Baada ya miezi nane, nilipangiwa kwenda kwenye kitengo kaskazini magharibi mwa Saigon. Wakati nikiwa huko, haraka niligundua kwamba mmoja wa wanahema wenzangu, Thomas Salisbury, alikuwa tofauti na kila mtu.

Tofauti hiyo ilikuwa wazi sana kwamba hatimaye nilimuuliza, “Tom, kwa nini wewe uko tofauti sana na kila mtu?”

“Kwa sababu mimi ni Mtakatifu wa Siku za Mwisho,” alijibu.

“Mtakatifu wa Siku za Mwisho ni nani?” Niliuliza.

Alifanya mpango kwa ajili yangu kukutana na yeye pamoja na Halord Lewis, mmisionari aliyerejea ambaye alikuwa anatumikia kama msaidizi wa kasisi wa kitengo. Wakati wa mkutano wetu wa kwanza katika hema ambalo lilitumika kama kanisa dogo, nilikubali kwamba kama hakika ningeamini kile walichokuwa wakiniambia, ningebatizwa. Pia nilipokea nakala ya Kitabu cha Mormoni, ambacho nilikiweka kwenye mfuko wa chini wa suruali yangu na kukisoma wakati nilipopata muda.

Mazungumzo kadhaa yalifuatia, na nilipata kwamba kila somo lilijibu maswali niliyokuwa nayo katika utafutaji wangu wa ukweli. Lakini wakati Tom na Harold waliponiuliza ikiwa nilitaka kubatizwa, nilisema la. Sikujua ni kwa jinsi gani ningeweza kushika amri zote walizokuwa wamenifundisha.

Baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa wilaya huko Saigon, nilienda Australia kwa ajili ya wiki ya mapumziko na kujiburudisha. Nikiwa huko, nilianza kutambua jinsi mafundisho ya injili yalivyokuwa muhimu kwangu. Niliporudi Vietnamu, mara moja nilimtangazia Tom kwamba ningependa kubatizwa.

Punde baadaye, Tom alinibatiza katika Ziwa Sông Bé, naye Harold akanithibitisha kama muumini wa Kanisa, na Timothy Hill, kiongozi wetu wa kundi wa Kanisa, alinitawaza kama shemasi.

Niliporudi nyumbani Marekani wiki sita baadaye, nilitambulisha injili kwa mpenzi wangu, ambaye alikuja kuwa mke wangu. Yeye pia aliukumbatia ujumbe wa injili uletao tumaini.

Daima nitakuwa mwenye shukrani kwamba Tom aliniuliza kama nilitaka kujua zaidi. Mfano wake na mwaliko ulijibu tamanio langu la kupata ukweli na kufurahia baraka za injili.