2023
Ni kwa Jinsi Gani Ninarahisisha Maisha Yangu Ili Kufokasi kwa Kristo?
Septemba 2023


Ni kwa Jinsi Gani Ninarahisisha Maisha Yangu Ili Kufokasi kwa Kristo? Liahona, 2023.

Njoo, Unifuate

2 Wakorintho 8–13

Ni kwa Jinsi Gani Ninarahisisha Maisha Yangu Ili Kufokasi kwa Kristo?

Picha
Yesu anatazama wakati watu wakilishwa

Wote Wakajazwa, na Walter Rane; picha ya lenzi ya kukuza vitu kutoka Getty Images

Mtume Paulo anatufundisha kufokasi kwenye “unyofu na usafi kwa Kristo” (2 Wakorintho 11:3).

Je, umewahi kujikuta ukifanya injili ya Yesu Kristo kuwa ngumu zaidi ya vile ilivyo? Wakati mwingine tunafokasi sana kwenye mwonekano wa nje au utondoti mdogo kiasi kwamba tunaanza kuhisi kuzidiwa.

Rahisisha Mtazamo Wako

Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anatoa pendekezo hili: “Kama uliwahi kufikiria kwamba injili haifanyi kazi vizuri kwako, ninakuomba rudi nyuma, yaangalie maisha yako kutokea sehemu ya juu, na rahisisha mwenendo wako wa ufuasi. Zingatia katika mafundisho ya msingi, kanuni, na matumizi ya injili. Ninawaahidi kwamba Mungu atawaongoza na kuwabariki katika njia zenu za maisha ya kuridhisha, na injili itafanya kazi vizuri kwenu” (“Inafanya kazi Vizuri Sana,” Liahona, Nov. 2015, 22).

Ni fundisho gani la msingi, kanuni, au matumizi ya injili ambayo ungefokasi juu yake wiki hii?