Muziki
Tenda Mema


133

Tenda Mema

Kwa uthabiti

1. Tenda mema; imeanza siku,

Mwanga na uhuru vyaingia.

Na malaika waandika juu

Kila tendo, hivyo tenda mema.

[Chorus]

Tenda mema; matokeo badaye.

Kwa nguvu uhuru pigania;

Kwa moyo shupavu uendelee.

Mungu yupo, hivyo tenda mema!

2. Tenda mema; zafunguka pingu.

Wafungwa uhuru wamepata.

Kwa imani hawana maumivu.

Ukweli wasonga; tenda mema.

[Chorus]

Tenda mema; matokeo badaye.

Kwa nguvu uhuru pigania;

Kwa moyo shupavu uendelee.

Mungu yupo, hivyo tenda mema!

3. Tenda mema; uoga uache.

Songa mbele, lengo waliona.

Nayo machozi yatakwisha punde.

Kuna baraka kutenda mema.

[Chorus]

Tenda mema; matokeo badaye.

Kwa nguvu uhuru pigania;

Kwa moyo shupavu uendelee.

Mungu yupo, hivyo tenda mema!

Maandishi: Hajulikani, The Psalms of Life, Boston, 1857

Muziki: George Kaillmark, 1781–1835

Kumbukumbu la Torati 6:17–18

Helamani 10:4–5