Muziki
Sifa Kwa Bwana, Mwenyezi


33

Sifa Kwa Bwana, Mwenyezi

Kwa shangwe

1. Sifa kwa Bwana, Mwenyezi, Mfalme wa mbingu!

O! Nafsi msifu aliye wokovu wangu!

Jumuika

Kwa zeze na kinanda,

Imbeni kwa kumwabudu!

2. Sifa kwa Bwana! Atawala kwa utukufu.

Kwenye mabawa huchukua Watakatifu.

Hujaona

Mahitaji kakupa

Alichokiweka wakfu?

3. Sifa kwa Bwana, mlinzi akuwezeshaye.

Hakika fadhila yake daima i nawe.

Tafakari

Uwezo wa Mwenyezi,

Rafiki akupendaye.

4. Sifa kwa Bwana! O! Nafsi yangu umwabudu!

Wote ungana na Abrahamu kumwabudu!

Na “amina!”

Zijumlishe sifa,

Sasa tunapoabudu.

Maandishi: Joachim Neander, 1650–1680; yalitafsiriwa na Catherine Winkworth, 1829–1878

Muziki: Kutoka Stralsund Gesangbuch, 1665; umepangiliwa na William S. Bennett, 1816–1875, na Otto Goldschmidt, 1829–1907

Zaburi 150

Zaburi 23:6