Muziki
Angazia


46

Angazia

Kwa sala

1. Niangaze kwenye giza hili.

Niongoze!

Ni usiku, na nyumbani mbali;

Niongoze!

Nioneshe njia ya kupita

Hata hatua moja yatosha.

2. Sikuwa hivi, na sikuomba

Niongozwe.

Nilipenda njia zangu; sasa,

Niongoze!

Nilipenda raha, bila hofu,

Nisamehe kwa kiburi changu.

3. Umenibariki na hakika

Upo nami—

Kwenye mito, mabonde, milima,

Na mauti.

Na kukicha nitatabasamu,

Na wapendwa, wale wafu wangu!

Maandishi: John Henry Newman, 1801–1890

Muziki: John B. Dykes, 1823–1876

Zaburi 43:3

Zaburi 119:133–135