Muziki
Iwe Upendavyo, Baba


102

Iwe Upendavyo, Baba

Kwa kutafakari

1. Alipokuwa mbinguni

Bwana aliteuliwa

Kuokoa wenye dhambi;

“Iwe upendavyo, Baba.”

2. Mtawala na Mfalme

Mnyenyekevu akawa,

Wakati na hali zote;

“Iwe upendavyo, Baba.”

3. Si miiba, si kejeli

Kristo zingemzuia.

Hakujali yake nafsi;

“Iwe upendavyo, Baba.”

4. Mkate nacho kikombe,

Ni kumbukumbu ya Bwana.

Tuombe nguvu tuseme,

“Iwe upendavyo, Baba.”

Maandishi: Frank I. Kooyman, 1880–1963. © 1948 IRI

Muziki: Robert P. Manookin, 1918–1997. © 1985 IRI

Musa 4:2

Luka 22:41–44

2 Nefi 10:24