Muziki
Yesu Ninapokuwaza


73

Yesu Ninapokuwaza

Kwa unyenyekevu

1. Yesu ninapokuwaza

Nafurahi mno;

Na nitafurahi hasa

Nikikaa kwako.

2. Hakuna cha kukumbuka,

Wala jina tamu,

Jema na lenye baraka,

Kama lako Yesu!

3. Kwa wote wanyenyekevu,

Huwapa furaha,

Mkarimu kwa waovu

Wakikurudia!

4. Yesu, u furaha yetu,

U zawadi pia,

Ndiwe utukufu wetu,

Sasa na daima.

Maandishi: Yanahusishwa na Bernard wa Clairvaux, mnamo 1091–1153; yametafsiriwa na Edward Caswall, 1814–1878

Muziki: John B. Dykes, 1823–1876

Zaburi 104:34

Enoshi 1:27