2021
COVID-19 na Mahekalu
Mei 2021


“COVID-19 na Mahekalu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumapili Alasiri

COVID-19 na Mahekalu

Dondoo

Picha
hekalu

Mapema mwaka jana, kwa sababu ya janga la ulimwengu la COVID-19 na hamu yetu ya kuwa raia wema ulimwenguni, tulifanya maamuzi magumu ya kufunga mahekalu yote kwa muda. Katika kipindi cha miezi iliyofuatia, tumehisi kupata mwongozo wa kiungu wa kufungua mahekalu pole pole kupitia hatua za tahadhari sana. Mahekalu sasa yanafunguliwa katika awamu nne, yakifuata kikamilifu kabisa taratibu za kiserikali za maeneo husika na itifaki za kiusalama. …

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na huduma ya kujitolea wakati huu wa kipindi cha mabadiliko na chenye changamoto. Ninaomba kwamba hamu yenu ya kuabudu na kuhudumu katika hekalu itawaka kwa uangavu zaidi sasa kushinda wakati wowote ule.

Yawezekana mnajiuliza ni lini mtaweza kwenda tena hekaluni. Jibu: Hekalu lenu litafunguliwa wakati taratibu za serikali yenu zitakaporuhusu.

Kwa sasa, shikeni maagano yenu ya hekaluni na mtapokea baraka akilini na mioyoni mwenu. Bakieni wakweli kwenye maagano ambayo mmeyafanya.

Tunajenga sasa kwa ajili ya siku za baadae! …

Tunataka kuileta nyumba ya Bwana hata jirani zaidi na waumini wetu, ili waweze kupata nafasi takatifu ya kuhudhuria hekaluni mara kwa mara kadiri hali zao zinavyowaruhusu. …

Mahekalu ni sehemu muhimu ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika utimilifu wake. Ibada za hekaluni zinajaza maisha yetu kwa nguvu na uwezo usiopatikana kwa njia nyingine yo yote. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya baraka hizi.