2021
Kaburi Halina Ushindi
Mei 2021


“Kaburi Halina Ushindi,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Kaburi Halina Ushindi

Dondoo

Picha
Yesu Kristo

Wakati fulani katika maisha yetu, tutakuwa tumehisi kuvunjika moyo baada ya kumpoteza mtu ambaye tunampenda sana. Kupitia janga la sasa la ulimwengu, wengi wetu wamepoteza wapendwa wao—wanafamilia au marafiki. Tunawaombea wale ambao wanahuzunika kwa upotevu kama huo. …

Tunaweza kufikiria jinsi marafiki wa Yesu, ambao walikuwa wamemfuata na kumtumikia Yeye, walivyojisikia wakati wa kushuhudia kifo Chake. Tunajua kwamba “waliomboleza na kulia.” [Marko 16:10]

… Nilipokuwa na umri wa miaka tisa, nilimpoteza kaka yangu mkubwa wakati wa tetemeko la ardhi haribifu. Kwa sababu ilitokea bila kutarajia, ilinichukua muda kuelewa ukweli wa kile kilichotokea. Niliumia sana moyoni kwa huzuni, na nilijiuliza, “Ni nini kilimtokea kaka yangu? Je, yuko wapi? Je, alikwenda wapi? Je, nitamwona tena?” …

Karibu miaka 40 baadaye, wakati wa Pasaka, nilikuwa nikitafakari juu ya Ufufuo wa Yesu Kristo na nikaanza kufikiria juu ya kaka yangu. …

Siku hiyo niligundua kuwa Roho alikuwa amenipa faraja katika wakati mgumu. Nilikuwa nimepokea ushuhuda kwamba roho ya kaka yangu haikufa; yuko hai. Bado anaendelea katika uwepo wake wa milele. Sasa ninajua kwamba “kaka [yangu] atafufuka tena” [Yohana 11:23] katika wakati huo adhimu, kwa sababu ya Ufufuko wa Yesu Kristo, sisi sote tutafufuliwa.