2021
Bariki katika Jina Lake
Mei 2021


“Bariki katika Jina Lake,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Ukuhani

Bariki katika Jina Lake

Dondoo

Picha
mvulana akipitisha sakramenti

Kusudi la kupokea kwetu ukuhani ni kuturuhusu sisi kuwabariki watu kwa niaba ya Bwana, tukifanya hivyo katika jina Lake.

Ilipita miaka mingi baada ya kuwa shemasi nilipopata kujifunza maana ya hili kwa vitendo. Kwa mfano, kama kuhani mkuu, nilipewa jukumu la kutembelea mkutano wa sakramenti katika kituo cha kulelea wazee. Niliombwa kupitisha sakramenti. Badala ya kufikiria kuhusu mchakato au umakini wa njia niliyopitisha sakramenti, nilitazama sura ya kila kikongwe. Niliona wengi wao wakilia. Mwanamke mmoja alishika mkono wa shati langu, akainua uso wake na kusema kwa sauti, “Ee, Asante, asante.”

Bwana alikuwa amebariki huduma yangu iliyotolewa katika jina Lake. Siku hiyo nilikuwa nimeomba kwa ajili ya muujiza kama huo kuja badala ya jinsi nitakavyofanya vyema sehemu yangu. Niliomba kwamba watu wangehisi upendo wa Bwana kupitia huduma yangu ya upendo. Nimejifunza huu ndio ufunguo wa kuwahudumia na kuwabariki wengine katika jina Lake. …

Ninaamini kwamba tunaweza kukuza huduma yetu ya ukuhani katika maisha yetu yote na labda hata zaidi ya hapo. Itategemea bidii yetu katika kujaribu kujua mapenzi ya Bwana na juhudi zetu za kusikia sauti Yake ili kwamba tuweze kujua vyema zaidi kile Yeye anataka kwa ajili ya mtu yule tunayemtumikia kwa ajili Yake. Ukuzaji huo utakuja katika hatua ndogo ndogo. Unaweza kuja pole pole, lakini utakuja.