2021
Unaweza Kuikusanya Israeli!
Mei 2021


“Unaweza Kuikusanya Israeli!,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Ukuhani

Unaweza kuikusanya Israeli!

Dondoo

Picha
kijana akipanda kilima

Takribani miaka mitatu iliyopita, Rais Russell M. Nelson aliwaalika vijana wote wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kujiandikisha katika “kikosi cha Bwana cha jeshi la vijana ili kusaidia kuwakusanya Israeli” pande zote mbili za pazia. Yeye alisema, “Ukusanyaji huo ni kitu muhimu zaidi kinachotokea duniani hii leo” [“Hope of Israel” (worldwide youth devotional, June 3, 2018), 8, HopeofIsrael.ChurchofJesusChrist.org]. Nina hakika kabisa wewe kijana unaweza kufanya hili—na ukafanya vizuri sana—kwa sababu ya (1) kitu kinachohusu utambulisho wako na (2) ni nguvu kubwa iliyoko ndani yako.

… Kulingana na kitabu cha Ufunuo, “kulikuwa na vita mbinguni”! [Ufunuo wa Yohana 12:7–8]. Shetani kwa ujanja alidanganya sehemu ya tatu ya watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni ili wamuache yeye ashinde badala ya Mungu. Lakini sio wewe! Mtume Yohana aliona kwamba ulimshinda Shetani “kwa neno la ushuhuda [wako].”… [Ufunuo 12:11].

… Kujua ulimshinda Shetani kwa neno la ushuhuda wako zamani kutakusaidia “kupenda, kushiriki, na kualika” sasa na siku zote—kuwaalika wengine waje na kuona, kuja na kusaidia, na kuja na kuwa sehemu ya, kama vita ile ile kwa ajili ya nafsi za watoto wa Mungu inaendelea. …

Programu ya Watoto na Vijana ni zana ya kinabii ili kukusaidia wewe kijana kuimarisha imani yako kubwa. … Vijana mnapoongoza —ongozeni— katika kuishi injili, kuwajali wengine, kuwaalika wote kupokea injili, kuunganisha familia milele, na kuandaa shughuli za kuburudisha, imani kubwa katika Kristo mliyokuwa nayo kabla ya maisha haya ya duniani itajitokeza na kuwapa nguvu ya kufanya kazi ya Bwana katika maisha haya!