2021
Tazama! Mimi ni Mungu wa Miujiza
Mei 2021


“Tazama! “Mimi ni Mungu wa Miujiza,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumapili Alasiri

“Tazama! Mimi ni Mungu wa Miujiza”

Dondoo

Picha
mandhari ya mlima

Miujiza, ishara, na maajabu ni mengi miongoni mwa wafuasi wa Yesu Kristo leo, katika maisha yako na yangu. Miujiza ni matendo ya kiungu, madhihirisho na maonyesho ya nguvu ya Mungu isiyo na kikomo na uthibitisho kwamba Yeye “ni yule yule jana, leo, na hata milele.”Moroni 10:19 Yesu Kristo, aliyeziumba bahari, anaweza kuzituliza; Yeye ambaye amewapa vipofu kuona anaweza kuinua macho yetu kuelekea mbinguni; Yeye aliyewatakasa wenye ukoma anaweza kutibu udhaifu wetu; Yeye aliyemponya yule mtu aliyepooza anaweza kutuita tuamke kwa “Njoo, unifuate.” [Luka 18:12].

Wengi wenu mmeshuhudia miujiza, zaidi ya jinsi mnavyotambua. Inaweza kuonekana kuwa midogo ikilinganishwa na Yesu kufufua wafu. Lakini ukubwa hautofautishi muujiza, ni kwamba tu umetoka kwa Mungu.

Kuna nyakati tunatarajia muujiza wa kumponya mpendwa wetu, kurudisha nyuma kitendo kisicho cha haki, au kulainisha moyo wenye chuki au nafsi iliyokata tamaa. Tukiangalia vitu kupitia macho ya kidunia, tunataka Bwana aingilie kati, kurekebisha kile kilichovunjika. Kupitia imani, muujiza utakuja, ingawa sio lazima kwenye ratiba yetu au kwa azimio tulilotamani. …

Bwana Ametukumbusha, “wala njia zenu si njia Zangu” [Isaya 55:8]. Anatuambia, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” [Mathayo 11:28]—ondoeni wasiwasi, kukata tamaa, hofu, kutokuamini, wasiwasi kuhusu wapendwa wenu, kwa ndoto zilizopotea au kuvunjika. Amani katikati ya kukanganyikiwa au huzuni ni muujiza.