2021
Yasiyo Haki Yenye Kughadhabisha
Mei 2021


“Yasiyo Haki Yenye Kughadhabisha,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Mei 2021

Kikao cha Jumamosi Alasiri

Yasio Haki Yenye Kughadhabisha

Dondoo

Picha
Yesu Kristo

Yasiyo haki yanaweza kuonekana kutoshabihiana na uhalisia wa Baba wa Mbinguni aliye mkarimu na mwenye upendo. Lakini bado Yeye ni halisi, mwema, na anampenda kila mmoja wa watoto Wake kwa ukamilifu. …

Baadhi ya kukosekana kwa usawa hakuwezi kuelezeka; kukosekana kwa usawa kusikofafanuliwa kunaghadhabisha. Maisha ya duniani kwa asili hayana usawa. …

… Natamka kwa uchungu wa moyo wangu wote kwamba Yesu Kristo anaelewa ukosefu wa haki na anao uwezo wa kutoa tiba. … Kwa ukamilifu kabisa Yeye anaelewa tunayoyapitia. …

… Katika umilele, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watamaliza kukosekana kote kwa haki. Tunaelewa kuwa sisi tunataka kujua kwa namna gani na lini. Ni kwa namna gani Wao watafanya hivyo? Lini Watafanya hivyo? Kwa ufahamu wangu, Wao bado hawajafunua namna au lini. Kitu ninachojua ni kwamba Wao watafanya. …

Tunaweza kujaribu kuzuia maswali yetu kuhusu ni kwa namna gani na lini kwa ajili ya baadae na kufokasi katika kukuza imani yetu katika Yesu Kristo.

Tunapokuza imani katika Yesu Kristo, tunapaswa pia kujitahidi kuwa kama Yeye. Kisha tunawatendea wengine kwa huruma na kujaribu kuondoa kukosekana kwa haki pale tunapouona. …

Usiache ukosefu wa haki ukufanye wewe kuwa mgumu, au kuharibu imani yako kwa Mungu. Badala yake, mwombe Mungu msaada. Ongeza shukrani yako kwa ajili ya na utegemezi wako kwa Mwokozi.

Imani yako kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo itapewa thawabu kuliko unavyoweza kufikiria. Yote yasiyo haki—hususani ukosefu wa haki kunaoghadhabisha—kutawekwa wakfu kwa faida yako.