2021
Chumba ndani ya Nyumba ya Wageni
Mei 2021


“Chumba Ndani ya Nyumba ya Wageni,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Chumba ndani ya Nyumba ya Wageni

Dondoo

Picha
Msamaria Mwema

Katika msimu huu wa Pasaka, Yesu Kristo anatualika sisi kuwa kama Yeye alivyo, Msamaria mwema, kuifanya nyumba Yake ya Wageni (Kanisa Lake) kuwa kimbilio kwa ajili ya wote kutokana na majeraha na dhoruba za maisha. …

Tunapokuja pamoja na Msamaria Mwema kwenye nyumba ya wageni, tunajifunza mambo matano kuhusu Yesu Kristo na sisi wenyewe.

Kwanza, tunakuja kwenye nyumba ya wageni kama tulivyo, tukiwa na kasoro za kiasili za mwanadamu na mapungufu kila mmoja wetu aliyonayo. Bado, kila mmoja wetu anacho kitu fulani anachohitajika kuchangia. Safari yetu hadi kwa Mungu daima inapatikana kwa pamoja. …

Pili, Yeye anatusihi sisi kuifanya hoteli Yake kuwa mahali pa neema na pa nafasi, mahali ambapo kila mmoja anaweza kukusanyika, kukiwa na nafasi kwa ajili ya wote. Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, wote tuko sawa, pasipo kuwa na makundi ya daraja la pili. …

Tatu, katika nyumba Yake ya wageni, tunajifunza ukamilifu u katika Yesu Kristo, si katika ukamilifu wa kiulimwengu. … Anatualika kila mmoja kuwa Msamaria mwema, mwenye kuhukumu kidogo na mwenye kuwasamehe wengine na kusameheana sisi kwa sisi. …

Nne, … Yeye anatuleta kwenye nyumba Yake ya wageni na pia kwenye nyumba Yake—hekalu takatifu … mahali ambapo … Msamaria huyu Mwema anaweza kutuosha na kutuvika, kututayarisha sisi kurudi kwenye uwepo wa Mungu, na kutuunganisha milele katika familia ya Mungu. …

Tano na mwisho, tunafurahi kwamba Mungu anawapenda watoto Wake katika asili na hali tofauti, katika kila taifa, kabila na lugha na ameweka nafasi kwa ajili ya wote katika nyumba Yake ya wageni.

Msamaria Mwema wetu anaahidi kurudi. Miujiza hutokea tunapojaliana kama ambavyo Yeye angefanya.