2021
Frederick M. Kamya
Septemba/ Oktoba 2021


WASIFU WA SABINI WA ENEO

Frederick M. Kamya

Frederick M. Kamya aliitwa kama Sabini wa Eneo mnamo Aprili 2021. Mzee Kamya anatokea Kampala, Uganda. Amekuwa Mkurugenzi Msimamizi wa kampuni ya uchapishaji ya Horizon Lines Ltd, tangu 1994. Yeye na mkewe Stella pia ni wakurugenzi wenza wa Victoria Meadows, kampuni ambayo inasimamia viwanda vidogo vidogo vya kilimo ikiwa ni pamoja na ufugaji na kilimo cha miti ya mbao.

Alikuwa Katibu Mkuu wa Uganda Printers Association kwa miaka 14, mpaka 2017. Alikuwa pia Rais wa Klabu ya Wanabiashara wa Kampala mnamo 2017/2018 na sasa ni Mwenyekiti wa Klabu ya Lubya investment.

Kabla ya wito wake kama Sabini wa Eneo, Alikuwa akihudumu kama Rais wa Kigingi cha Kampala Uganda South. Miito yake ya awali inajumuisha kuhudumu kama Rais wa Tawi, Askofu, Mshauri wa Urais wa Wilaya na Rais wa Wilaya.

Mzee Kamya ana Shahada ya Ualimu, pamoja na Stashahada. Yeye pamoja na mkewe Stella ni wazazi wa watoto sita. Kwa sasa wanaishi Kampala.

Mzee Kamya anasema kwamba ana shukrani kwa Bwana kwa wito huu na ana shauku ya kujifunza jukumu lake, ili kwamba aweze kuwa mtumishi bora zaidi wa Bwana kadiri awezavyo. Anatumaini na kuomba kwamba kwa kufanya hivyo aweze kugusa maisha ya watu.