2021
Ukweli Safi, Mafundisho Safi, na Ufunuo Safi
Novemba 2021


“Ukweli Safi, Mafundisho Safi, na Ufunuo Safi,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Ukweli Safi, Mafundisho Safi, na Ufunuo Safi

Dondoo

Akina kaka na dada zangu wapendwa, karibuni kwenye mkutano mkuu! …

… Ninawaalikeni kusikiliza vitu vitatu wakati wa mkutano huu: ukweli halisi, injili halisi ya Kristo na ufunuo halisi. Kinyume na mashaka ya baadhi yenu kuna kitu kama hicho cha ukweli na uongo. Kweli kuna ukweli halisi—ukweli wa milele. Mojawapo wa majanga ya siku yetu ni kwamba watu wachache wanajua wapi pa kugeukia kwa ajili ya ukweli. Nawahakikishieni kwamba mtakachokisia leo na kesho kinabeba ukweli halisi.

Injili halisi ya Kristo ina nguvu. Inabadilisha maisha ya kila mtu ambaye anaielewa na kutafuta kuitenda katika maisha yake. Injili ya Kristo hutusaidia kupata na kubakia kwenye njia ya agano. Kubakia kwenye njia hiyo nyembamba lakini iliyo na mpangilio hatimaye kutatuwezesha kupokea vitu vyote alivyonayo Mungu. Hakuna chenye thamani zaidi ya vyote alivyonavyo Baba yetu!

Hatimaye, ufunuo halisi kwa ajili ya maswali ndani ya moyo wako utafanya mkutano huu kuwa wenye thawabu na usiosahaulika. Kama bado hujatafuta kuhudumiwa na Roho Mtakatifu ili akusaidie kusikia kile Bwana angetaka ninyi msikie katika siku hizi mbili, nawaalika kufanya hivyo sasa. Tafadhali fanyeni mkutano huu kuwa muda wa kusherehekea katika jumbe kutoka kwa Bwana kupitia watumishi Wake. Jifunzeni jinsi ya kutumia jumbe hizo maishani mwenu.