2021
Tenga Muda kwa ajili ya Bwana
Novemba 2021


“Tenga Muda kwa ajili ya Bwana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Alasiri

Tenga Muda kwa ajili ya Bwana

Dondoo

Picha
wachungaji

Sauti na mashinikizo ya ulimwengu ni ya kuvutia na ni mengi. Lakini sauti nyingi sana ni za uongo, zenye kuhadaa, na zinaweza kutuvuta kutoka kwenye njia ya agano. Ili kuepuka kuvunjika moyo kusikoepukika kunakofuatia, ninawasihi leo kupambana na mitego na majaribu ya ulimwengu kwa kutenga muda kwa ajili ya Bwana katika maisha yenu—kila siku ipitayo.

Ikiwa wingi wa taarifa unazopata zinatoka kwenye mitandao ya kijamii au mingine, uwezo wako wa kusikia minong’ono ya Roho utapungua. Ikiwa pia humtafuti Bwana kupitia sala na usomaji wa injili kila siku, unajiacha kuwa muhanga wa filosofia ambazo zinaweza kuwa za kuvutia lakini si za kweli. Hata Watakatifu ambao pengine waaminifu wanaweza kuvutiwa na mdundo wa mara kwa mara wa bendi ya Babeli.

Kaka zangu na dada zangu, ninawasihi mtenge muda kwa ajili ya Bwana! Fanya msingi wako mwenyewe wa kiroho kuwa imara na unaoweza kuhimili majaribu ya kila wakati kwa kufanya mambo yale ambayo yanamruhusu Roho Mtakatifu kuwa pamoja nawe daima. …

Hakuna kinachomwalika Roho zaidi ya kukita fokasi yako juu ya Yesu Kristo. Zungumzeni kuhusu Kristo, furahieni katika Kristo, kuleni na kusherehekea maneno ya Kristo na msonge mbele mkiwa na uimara katika Kristo. Ifanyeni Sabato yenu kuwa ya furaha pale mnapomwabudu Yeye, kupokea sakramenti na kuifanya siku Yake kuwa takatifu.

Kama nilivyosisitiza asubuhi ya leo, tafadhali tengeni muda kwa ajili ya Bwana katika nyumba Yake takatifu. …

… Atakuelekeza na kukuongoza wewe katika maisha yako binafsi ikiwa utatenga muda kwa ajili Yake katika maisha yako—kila siku ipitayo.