2021
Ustahili Si Kukosa Dosari
Novemba 2021


“Ustahili Si Kukosa Dosari,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov 2022.

Kikao cha Jumamosi Jioni

Ustahili Si Kukosa Dosari

Dondoo

Picha
wanaume wakikumbatiana

Wengine kimakosa wanapokea ujumbe kwamba toba na badiliko havina haja. Ujumbe wa Mungu ni kwamba ni vya muhimu. …

Baadhi kimakosa hupokea ujumbe kwamba toba ni tukio la mara moja. Ujumbe wa Mungu ni kwamba, kama ambavyo Rais Russell M. Nelson amefundisha “Toba … ni mchakato.” …

Baadhi kimakosa wanapokea ujumbe kwamba hawastahili kushiriki kikamilifu katika injili kwa sababu hawako huru kikamilifu kutokana na mazoea mabaya. Ujumbe wa Mungu ni kwamba ustahili si kukosa dosari. Ustahili ni kuwa mwaminifu na mwenye kujaribu. Ni lazima tuwe waaminifu kwa Mungu, viongozi wa ukuhani, na wengine ambao wanatupenda, na lazima tujitahidi kushika amri za Mungu na kamwe tusife moyo kwa sababu tu tumeteleza. …

Baadhi kimakosa wanapokea ujumbe kwamba Mungu anangojea kutusaidia mpaka baada ya kuwa tumetubu. Ujumbe wa Mungu ni kwamba Yeye daima atatusaidia wakati tunapotubu. …

… Neema Yake si tu tuzo kwa wale wenye kustahili. Ni “msaada wa kiungu” ambao Yeye hutoa ambao hutusaidia kuwa wastahili. Si tu zawadi kwa watu wema. Ni “endaomenti ya nguvu” ambayo Yeye hutoa ambayo hutusaidia kuwa wema. Sisi hatutembei tu kuwaelekea Mungu na Kristo. Tunatembea pamoja Nao. …

Wakati unapohisi kuwa umeshindwa mara nyingi kuendelea kujaribu, kumbuka Upatanisho wa Kristo na neema utoayo ni halisi. “Mikono [Yake] ya rehema imenyoshwa kukuelekea wewe” [3 Nefi 9:14]. Wewe unapendwa—leo, katika miaka 20, na milele.