2021
Imani ya Kuuliza na Kisha Kutenda
Novemba 2021


“Imani ya Kuuliza na Kisha Kutenda,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Jioni

Imani ya Kuuliza na Kisha Kutenda

Dondoo

Picha
Mtu akisali

Njia ya kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu haijabadilika kutoka siku za Adamu na Hawa. Imekuwa vivyo hivyo kwa watumishi wote walioitwa na Bwana kutoka mwanzo mpaka siku ya leo. Ndivyo ilivyo kwenu na kwangu. Hili hufanyika daima kwa kuonyesha imani. …

… Una maswali ambayo unatafuta majibu. Unayo angalau imani ya kutosha ya kutegemea kwamba utapokea majibu kutoka kwa Bwana kupitia watumishi Wake. Hutakuwa na fursa ya kuuliza kwa sauti kwa ajili ya majibu kutoka kwa wanenaji, bali unaweza kumwuliza Baba yako mwenye upendo katika sala.

Ninajua kutokana na uzoefu kwamba majibu yatakuja sawa na mahitaji yako na maandalizi yako ya kiroho. …

Kama imani yako katika Yesu Kristo imepelekea kwenye moyo kulainishwa kupitia matokeo ya Upatanisho Wake, utakuwa na uwezo zaidi wa kuhisi minong’ono ya Roho katika jibu kwa sala zako. …

Kwa vile imani yetu katika Yesu Kristo itakuwa imetuongoza kumwomba Baba majibu, imani hiyo pia itakuwa imeleta mguso wa Mwokozi wa kulainisha vya kutosha ili sisi kusikia mwongozo Wake na kuazimia na kusisimka kutii. …

Ni ushuhuda wangu kwamba mwamba tunaosimama juu yake ni ushuhuda wetu kwamba Yesu ndiye Kristo; kwamba hili ni Kanisa Lake, analoliongoza yeye binafsi; na kwamba Rais Russell M. Nelson ndiye nabii Wake aliye hai leo. …

Ninaomba kwamba muweze kuwa na ushahidi kama huo.