2021
Njoo kwa Kristo na Usije Peke Yako
Novemba 2021


“Njoo kwa Kristo na Usije Peke Yako,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Njoo kwa Kristo na Usije Peke Yako

Dondoo

Picha
Yesu Kristo

Je, umewahi kuhisi aina hiyo ya hisia, ukijiuliza kama Baba wa Mbinguni anakujua wewe ni nani na kama Anakuhitaji? Vijana wangu wapendwa, na kwa wote, ninashuhudia kuwa jibu ni ndio! Bwana ana Mpango na wewe! Yeye amekuandaa kwa ajili ya siku hii, hivi sasa, kuwa nguvu na ushawishi wa uzuri katika kazi Yake. Tunakuhitaji! Kiufupi haiwezi kuwa kuu bila ninyi!. …

… Njooni kwa Kristo Njoo sasa, lakini usije peke yako! …

Kumbuka, njia bora zaidi ya ninyi kuboresha ulimwengu ni kwa kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Kristo kwa kuwaalika wote kumfuata Yeye. …

Yeye anajua masumbuko yetu na mahangaiko vilevile na anatuita, Waleteni wenye wasiwasi na mvunjiko wa moyo, waliochoka, wenye majivuno na wasioeleweka, “wapweke, au wale ambao wanateseka kwa njia yoyote.”

… Ni nani utakayemleta kwa Kristo? Je, nani utamleta ? …

… Wasichana na wavulana, anzeni sasa, katika nyumba zenu …

Ni wakati mtukufu ulioje kujihusisha katika kazi ya Kristo!

Ndio, mko hapa kwa ajili ya kitu kikuu. Ninaungana na Rais Nelson, ambaye alisema: “Bwana anawahitaji ninyi muubadili ulimwengu. Mnapokubali na kufuata mapenzi Yake kwa ajili yenu, mtapajipata mkitimiza yasiyowezekana!” [Russell M. Nelson, Accomplishing the Impossible: What God Does, What We Can Do (2015), 147].