2021
Jina la Kanisa Si Jambo la Mjadala
Novemba 2021


“Jina la Kanisa Si Jambo la Mjadala,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Alasiri

Jina la Kanisa Si Jambo la Mjadala

Dondoo

Picha
mwanga unaoangaza ndani ya pango

Katika mkutano na wanahabari mnamo Agosti 16, 2018, Rais Russell M. Nelson alisema: “Bwana amesisitiza akilini mwangu umuhimu wa jina ambalo Amefunua kwa ajili ya Kanisa Lake, hata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho” [“The Name of the Church,” Aug. 16, 2018, newsroom.ChurchofJesusChrist.org]. …

Swali zuri likaibuka: Kwa nini sasa, wakati kwa miongo mingi tumelikubali jina la utani la “Mormoni”? “Kwaya ya Mormoni Tabenako,” video fupi za “Mimi ni Mmormoni,” wimbo wa Msingi “Mimi ni Mvulana Mmormoni”?

Mafundisho ya Kristo hayabadiliki na ni ya milele. Bali hatua mahususi na muhimu za kazi ya Mwokozi zinafunuliwa katika wakati ufaao. …

Asanteni kwa juhudi zenu za kiungwana kusongesha mbele jina la Kanisa.

Bwana amekuza juhudi zetu za kurekebisha majina ambayo kwa muda yalihusiana na Kanisa. …

Kuna maelfu na maelfu ya Watakatifu wa Siku za Mwisho ambao kwa ujasiri wametangaza jina la Kanisa. Tunapofanya sehemu yetu, wengine watafuata. …

“Jina la Kanisa si jambo la mjadala.” Acha tusonge mbele kwa imani. Wakati bila shuruti tunapofuata ushauri wa Bwana, kama ulivyofunuliwa kupitia nabii Wake aliye hai hususani ikiwa unapita fikra zetu za juu, ukihitaji unyenyekevu na dhabihu, Bwana anatubariki kwa nguvu za ziada za kiroho na kutuma malaika Zake ili watusaidie na kusimama nasi. Tunapokea uthibitisho wa Bwana na ukubali Wake.