2022
‘Kuisubiria siku yenyewe’: Jinsi waumini walivyojiandaa kwa ajili ya hekalu la DRC
Januari/Februari 2022


KURASA ZA ENEO

‘Kuisubiria siku yenyewe’: Jinsi waumini walivyojiandaa kwa ajili ya hekalu la DRC

Rais wa Hekalu la Kinshasa DRC anayemaliza muda wake anakumbuka msisimko na maandalizi ya watakatifu wakati hekalu lilipofunguliwa.

Mnara wa Nyumba ya Bwana unakaribia kufikia mbingu kwenye anga la jioni huko Kinshasa, DRC. Unaleta hisia ya amani na utulivu kwa wote wanaopita karibu na kuangalia viwanja vizuri vya hekalu. Kwa waumini ni ukumbusho wa kuhudhuria mara kwa mara, ili kuweka na kufanya upya maagano yao na Bwana, na kuhisi uwepo wa Bwana na ushauri katika maisha yao.

Mnamo tarehe 1, Oktoba 2011, Rais Thomas S. Monson (1927-2018) alitangaza kwamba hekalu la 163 ulimwenguni litajengwa huko Kinshasa, DRC. Rais Brent Jameson, Rais wa misheni ya Kinshasa wakati huo, anashiriki kumbukumbu hii:

“Kila baada ya wiki sita tulisafiri kwenye matawi na kata za kanisa zilizokuwa mbali. Huko Pointe Noire tulipokelewa na Rais wa Tawi ambaye alisema kuna waumini wachache ambao walihitaji vibali vya hekaluni na kwamba wote walikuwa wamejipanga mstari ndani ya kanisa. Kulikuwa na watu 16 waliokuwa wakisubiri kufanya upya au kupata vibali! Uzoefu huu ulijitokeza kila mahali tulipotembelea. Kwa dhabihu kubwa kipesa, kwa masaa mengi ya kusafiri, na si kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kufanya upya au kupata vibali, walikuwa wamekuja. Waumini hawa walielewa umuhimu wa kuwa na kibali hai. Walijua kinaonyesha kwa Bwana ni kwa dhati kiasi gani walikuwa wakiishi injili na jinsi maagano yao yalivyokuwa muhimu kwao. Walijua kwamba pengine wangeweza au wasingeweza kufika hekaluni, lakini walitaka kuwa tayari kuingia na kufanya maagano yao wakati wowote fursa itakapokuja. Vibali vyao vilimaanisha kitu muhimu kwao na kwa Bwana.”

Baadaye, mnamo 2018, Rais Jameson anashiriki uzoefu huu wa kihisia:

“Tuliitwa kama Rais na Matroni wa Hekalu la Kinshasa. Tulikuja mapema kwa lengo la kufanya usaili wa vibali ili kwamba wengi kadiri ambavyo ingewezekana wangekuwa tayari kuingia hekaluni. Tuliomba walioweza kujitolea kuhudumu kama wafanyakazi wa hekaluni. Mara moja kulikuwa na watu 250 waliojitolea na kila mmoja wao alikuwa na kibali hai cha hekaluni! Walikuwa tu wakiisubiria siku. Wengi walikuwa wamehudhuria hekaluni mara moja kwa ajili ya endaumenti zao—wengi walikuwa Maaskofu na Marais wa vigingi—lakini walikuwa hawajapata fursa ya kuhudhuria tena. Siku ilikuwa imefika kwa ajili ya kuhudhuria hekaluni mara kwa mara!”

Leo, Agosti 2021, Bwana ameita Urais mpya wa Hekalu kutoka miongoni mwa waumini wa Kikongo: Rais M. Francois Mukubu, Mshauri wa Kwanza Kabua K. Tshimungu, Mshauri wa Pili Jules Bofanga. Siku imewadia. Kama Rais Nelson asemavyo, “weka hekalu ndani yako na pia jiweke ndani ya hekalu.”