2022
Jinsi Kitabu cha Mwongozo Kinavyoweza Kukusaidia Ujifunze Zaidi kuhusu Wito Wako
Januari/Februari 2022


MAMBO MUHIMU YA KITABU CHA MWONGOZO

Jinsi Kitabu cha Mwongozo Kinavyoweza Kukusaidia Ujifunze Zaidi kuhusu Wito Wako

Moja ya vipengele vya kuridhisha vya kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni fursa kwamba utaweza kutumikia katika miito na majukumu. Haya ni majukumu ya kujitolea ambayo hujumuisha aina mbalimbali za huduma ndani ya Kanisa. Kwa mfano, unaweza kuitwa kama mwalimu wa Msingi, mshauri kwa Wavulana, karani katika urais wa tawi, katibu kwenye Urais wa Muungano wa Usaidizi wa Kigingi, mshauri katika urais wa Akidi ya Makuhani, mtaalamu wa teknolojia wa kata, au mwana historia kwa ajili ya tawi lako.

Baada ya kuwa umekubali wito wako, ukaidhinishwa na waumini wa kitengo chako na kutawazwa na viongozi wako wa ukuhani kwa kupokea baraka ya ukuhani, upo tayari kutumikia. Lakini unawezaje kujua kile kinachotarajiwa kutoka kwako na ni jinsi gani unaweza kukuza wito wako?

Bwana alifundisha, “Acha kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi katika ofisi ambayo ameteuliwa, kwa bidii yote” (ona Mafundisho na Maagano 107:99). Kama kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, unapaswa kutafuta ufunuo binafsi ili ukusaidie kujifunza na kutimiza majukumu ya wito wako.

Kujifunza maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho kutakusaidia kuelewa na kutimiza majukumu yako. Unapojifunza maneno ya Mungu, utakuwa msikivu zaidi kwa ushawishi wa Roho (ona Mafundisho na Maagano 84:85).

Unajifunza pia majukumu yako kwa kusoma maelekezo katika Kitabu cha Mwongozo. Maelekezo haya yanaweza kualika ufunuo ikiwa yatatumiwa kupata uelewa wa kanuni, sera na taratibu za kutumia wakati ukitafuta mwongozo wa Roho.