2023
Wapatanishi Wanahitajika
Mei 2023


Wapatanishi Wanahitajika

Dondoo

Picha
karatasi ya kupamba ukutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunapaswa kuwa mifano ya jinsi ya kuchangamana na wengine—hasa tunapokuwa na maoni tofauti. Njia mojawapo rahisi sana ya kumtambua mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni jinsi gani kwa huruma mtu huyo huwatendea watu wengine.

… Wafuasi Wake wa kweli wanawajenga, wanawainua, wanawatia moyo, wanawashawishi na kuwavutia wengine—bila kujali ugumu wa hali. Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni wapatanishi.

Upatanisho wa Yesu Kristo ulifanya iwezekane kwetu sisi kushinda uovu wote —ikijumuisha ubishi. …

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, jinsi gani sisi tunatendeana ndicho kitu cha muhimu hasa! Jinsi gani tunavyozungumza na wengine na kuhusu watu wengine nyumbani, kanisani, kazini na mtandaoni ni kitu muhimu zaidi. Leo, ninawaomba sisi tuchangamane na watu wengine katika njia ya hali ya juu na takatifu zaidi.

Hisani ni dawa ya ubishi. Hisani ni kipawa cha kiroho ambacho hutusaidia kumtupilia mbali mwanadamu wa asili, ambaye ni mbinafsi na mwenye kujitetea, mwenye kiburi na mwenye wivu. Hisani ni tabia ya msingi ya mfuasi halisi wa Yesu Kristo. Hisani humfafanua mpatanishi.

… Ninakualikeni mumkumbuke Yesu Kristo. Omba ili upate ujasiri na hekima ya kusema au kufanya kile ambacho Yeye angefanya. Tunapomfuata Mfalme wa Amani tutakuwa wapatanishi Wake. …

… Leo ninawaalika kutathmini ufuasi wenu katika muktadha wa jinsi mnavyowatendea wengine. Ninawabariki katika kufanya marekebisho ambayo yanaweza kuhitajika ili kwamba tabia yako iwe ya kuinua, ya heshima na ya kumwakilisha mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.