2023
Kuzifikia Nguvu za Mungu kupitia Maagano
Mei 2023


Kuzifikia Nguvu za Mungu kupitia Maagano

Dondoo

Picha
karatasi za kupamba ukkutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Kabla ya dunia kuumbwa, Mungu alianzisha maagano kama utaratibu ambao kupitia huo sisi, watoto Wake, tungeweza kujiunganisha Kwake. …

… Tunafanya agano pale tu tunapokusudia kujitoa kwa dhati kulitimiza. Tunakuwa watoto wa Mungu wa agano na warithi wa ufalme Wake, hasa pale tunapojitambulisha sisi wenyewe kikamilifu kwa agano.

Neno njia ya agano humaanisha mlolongo wa maagano ambayo kupitia kwayo tunakuja kwa Kristo na kuunganika Naye. Kupitia muunganiko huu wa agano, tunapata kuzifikia nguvu Zake za milele. Njia hii huanza na imani katika Yesu Kristo na toba, ikifuatiwa na ubatizo na kumpokea Roho Mtakatifu. …

Njia ya agano huongoza kwenye ibada za hekaluni, kama vile endaumenti ya hekaluni. Endaumenti ni zawadi ya Mungu ya maagano matakatifu ambayo hutuunganisha kikamilifu Kwake. …

Kushika maagano yaliyofanywa katika visima vya ubatizo na ndani ya mahekalu pia hutupatia nguvu ya kuhimili majaribu na maumivu ya maisha ya duniani. …

Unapotembea njia ya agano, kuanzia ubatizo hadi hekaluni na maisha yako yote, ninakuahidi nguvu ya kwenda dhidi ya mtiririko wa asili wa ulimwengu—nguvu ya kujifunza, nguvu ya kutubu na kutakaswa na nguvu ya kupata tumaini, faraja na hata shangwe wakati unapopitia changamoto za maisha. Ninakuahidi wewe na familia yako ulinzi dhidi ya ushawishi wa adui, hususani wakati hekalu ni fokasi kubwa katika maisha yako.