2023
Jibu Daima ni Yesu Kristo
Mei 2023


Jibu Daima ni Yesu Kristo

Dondoo

Picha
karatasi ya kupamba ukutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Wiki moja kutoka leo itakuwa Jumapili ya Pasaka. Haya ni maadhimisho muhimu sana ya kidini kwa wafuasi wa Yesu Kristo. Sababu muhimu ya kusherehekea Krismasi ni kwa sababu ya Pasaka. …

… Kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi tunaweza kutubu na kusamehewa dhambi zetu. Kwa sababu Yake, kila mmoja wetu atafufuka. …

… Ninawasihi mje Kwake ili kwamba Yeye aweze kuwaponya ninyi! Yeye atawaponya ninyi kutokana na dhambi mnapotubu. Yeye atawaponya ninyi kutokana na huzuni na hofu. Yeye atawaponya ninyi kutokana na majeraha ya ulimwengu huu.

Maswali au matatizo yoyote mliyonayo, jibu daima linapatikana katika maisha na mafundisho ya Yesu Kristo. Jifunzeni zaidi kuhusu Upatanisho Wake, upendo Wake, rehema Yake, mafundisho Yake, na injili Yake ya urejesho ya uponyaji na ukuaji. Mgeukieni Yeye! Mfuateni Yeye!

Yesu Kristo ni sababu ya sisi kujenga mahekalu. Kila moja ni nyumba Yake takatifu. Kufanya maagano na kupokea ibada muhimu katika hekalu, vile vile kutafuta kusogea karibu Naye hekaluni, kutabariki maisha yenu katika njia ambayo hakuna aina nyingine ya kuabudu inaweza. Kwa sababu hii, tunafanya yote yaliyo katika uwezo wetu kufanya baraka za hekalu kupatikana zaidi kwa waumini wetu kote ulimwenguni. …

Wapendwa kaka zangu na dada zangu, ninatoa ushahidi wangu kwamba Yesu Kristo anaelekeza kazi za Kanisa Lake. Ninashuhudia kwamba kumfuata Yeye ndiyo njia pekee ya furaha ya kudumu.