2023
Uhudumiaji
Mei 2023


Uhudumiaji

Dondoo

Picha
karatasi ya kupamba ukutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunatafuta kuwahudumia wengine kama ambavyo Yeye angefanya kwa sababu maisha yanasubiri kubadilishwa. …

Kila mahali ninapoenda, kwa shukrani ninajifunza kutoka kwa wale wanaohudumu na kujali kama ambavyo Mwokozi wetu angefanya. …

Uhudumiaji wa hali ya juu na takatifu huja tunaposali kwa ajili ya “upendo msafi wa Kristo”[ona Moroni 7:47–48] na kumfuata Roho. …

… Katika maeneo mengi, tunaweza kuwafikia, kuwaelewa wengine mahali walipo, na kujenga uhusiano wakati tunapowatembelea waumini mara kwa mara katika nyumba zao. Mialiko yenye mwongozo wa kiungu hubadili maisha. Wakati mialiko inapotusaidia kufanya na kushika maagano matakatifu, tunasonga karibu zaidi na Bwana na kila mmoja wetu. …

Uhudumiaji wenye mwongozo wa kiungu hubariki familia na watu binafsi; pia huimarisha kata na matawi. …

Mwokozi ndiye mfano wetu mkamilifu. Kwa sababu Yeye ni mwema, anaweza kwenda huku na huko akitenda mema. Yeye humbariki yule mmoja na wale 99. Yeye ni mfano binafsi wa uhudumiaji. …

Yesu Kristo anahudumia. Malaika wanahudumia. … Tunapohudumu kama ambavyo Yeye angehudumu, tunashuhudia miujiza Yake, baraka Zake. …

Popote tulipo wakati huu wa Pasaka, acha tufikie na kujali kama ambavyo Mwokozi wetu angefanya, hususani kwa wale ambao tumepata fursa kwa upendo na kwa jukumu kuwahudumia. Katika kufanya hivyo, na tusonge karibu zaidi na Yesu Kristo na kila mmoja wetu, tukiwa zaidi kama Yeye na wafuasi wa Yesu Kristo ambao Yeye angetaka kila mmoja wetu awe.