2023
Mafundisho ya Yesu Kristo
Mei 2023


Mafundisho ya Yesu Kristo

Dondoo

Picha
karatasi ya kupamba ukutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Kama nabii Nefi alivyotufundisha, tunapaswa “kusherehekea juu ya maneno ya Kristo; kwani tazama, maneno ya Kristo yatawaelezea vitu vyote mnavyostahili kutenda.”1 … Ujumbe wangu leo ni pamoja na uteuzi wa maneno ya Mwokozi wetu—kile Yeye alichosema. …

“[Amri kuu katika sheria ni hii:] mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

“Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

“Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

“Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”2 …

“Amin, amin, ninawaambia, lazima mjihadhari na kusali daima, msije mkajaribiwa na ibilisi, na mwongozwe mbali kama mateka wake.”3 …

“Kwa hivyo, chochote mtakachofanya, mfanye katika jina langu; kwa hiyo mtaita kanisa kwa jina langu.”4 …

“Sasa hii ndiyo amri: Tubuni, ninyi nyote katika sehemu zote za dunia, na mje kwangu na mbatizwe katika jina langu ili muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili muweze kusimama mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho.”5 …

Tunaamini katika Kristo. Ninahitimisha na kile Yeye alichokisema kuhusu namna ya kujua na kufuata mafundisho Yake:

“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”6