2023
Kumbuka Kile Kilicho Muhimu Zaidi
Mei 2023


Kumbuka Kile Kilicho Muhimu Zaidi

Dondoo

Picha
karatasi za kupamba ukkutani

Pakua karatasi ya kupamba ukutani

Leo, nitashiriki kutoka moyoni mwangu hisia na mawazo machache juu ya mambo yaliyo muhimu zaidi.

Kwanza, uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni na Mwanaye, Bwana Yesu Kristo, ni muhimu zaidi. Uhusiano huu ni muhimu zaidi sasa na milele.

Pili, uhusiano wa familia ni kati ya mambo yale yaliyo muhimu zaidi. …

Ninatambua baadhi inawezekana hawana baraka ya familia ya karibu, hivyo ninajumuisha familia zingine, marafiki na hata familia za kata au tawi kama “familia.” Uhusiano huu ni wa msingi kwa ajili ya afya ya kihisia na kimwili. …

Kitu kingine kilicho muhimu zaidi ni kufuata msukumo wa Roho katika uhusiano wetu muhimu zaidi na katika juhudi zetu za kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda, ikijumuisha katika huduma zetu za faragha na za umma. …

Mwisho, katika wikiendi hii ya Jumapili ya Matawi, ninashuhudia kwamba uongofu kwa Bwana, kushuhudia juu Yake na kumtumikia Yeye pia ni kati ya mambo yaliyo muhimu zaidi. …

Kuwa na ushuhuda peke yake haitoshi. Kadiri uongofu wetu kwa Yesu Kristo unavyokua, kwa kawaida huwa tunataka kushuhudia juu Yake—wema Wake, upendo na ukarimu Wake. …

Ninakualika utoe ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo mara kwa mara. …

Wale wanaohisi kitu kama matokeo ya ushuhuda wako wanaweza kumwomba Bwana katika sala ili athibitishe ukweli wa ushuhuda wako. Kisha wanaweza kujua wao wenyewe.