Liahona
Kanuni 3 Za Mwongozo kwa ajili ya Kutumia Teknolojia na Vyombo vya Habari
Machi 2024


Kanuni 3 Za Mwongozo kwa ajili ya Kutumia Teknolojia na Vyombo vya Habari,” Liahona, Machi, 2024.

Kanuni 3 Za Mwongozo kwa ajili ya Kutumia Teknolojia na Vyombo vya Habari

Wakati teknolojia inaendelea kukua, mitazamo hii ya vyombo vya habari itatusaidia tusonge mbele kwa busara.

Picha
mkono ukiwa umeshikilia simu janja yenye bodi ya saketi kwenye skrini.

Teknilojia inabadilika kila dakika. Na kila maendeleo katika teknolojia yameleta njia mpya za kutumia vyombo vya habari. Mashine ya uchapishaji ilibadilisha sana ni nani angeweza kupata maneno yaliyoandikwa. Redio na runinga vimebadilisha sana jinsi tunavyowasilisha habari, taarifa, na burudani. Intaneti imebadilisha kiasi gani cha maudhui tungeweza kupata na nani angeweza kuyatengeneza. Vyombo vya habari vimebadilisha uwezo wetu wa kupata, kuwasiliana, na kuunganika na watu. Kadiri akili bunifu zinavyojitokeza, tunakabiliwa na maswali mapya.

Teknolojia mpya kamwe siyo zote nzuri au zote mbaya. Badala yake, mara nyingi ni kama kioo kuzi ambacho kinaweza kukuza fursa mpya na shauku mpya. Tunapojitahidi kuwa zaidi kama Kristo, mwitikio wetu kwa teknolojia mpya na vyombo vya habari inavyoweza kuleta ndani ya maisha yetu ndicho kilicho muhimu.

Mbinu Iliyojikita kwenye Kanuni

Kwa vyovyote, hakuna orodha ya sheria kuongoza kila uamuzi tunaofanya kuhusu teknolojia na vyombo vya habari. Badala yake, tunaweza kujifunza kanuni ili kusaidia kutuongoza tunapofanya maamuzi. Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “Kanuni ni za milele na za mambo yote. Sheria mahususi au utumiaji wa sheria hizo hufanya kazi vizuri katika baadhi ya sehemu na kutofanya kazi sehemu zingine. Kile ambacho hutuunganisha ni Yesu Kristo na kweli za milele Yeye alizozifundisha, hata kama matumizi mahususi hutofautiana kwa muda mrefu na kwenye tamaduni.”1

Kufuata kanuni zenye msingi kwenye kweli za injili kutatusaidia tubaki kwenye njia ya agano. Roho atatuongoza tunapojitahidi kufanya chaguzi zenye msingi kwenye kanuni hizo. Kwa hiyo ni kanuni zipi zinaweza kusaidia kuongoza chaguzi zetu kuhusu teknolojia na vyombo vya habari?

1. Ninaweza kutumia uadilifu wangu wa haki ya kujiamulia kufanya chaguzi kuthibiti teknolojia. Teknolojia hainithibiti mimi.

Inaweza wakati mwingine kuonekana kama teknolojia inayapita maisha yako. Ni muhimu kukumbuka kwamba unaweza kufanya chaguzi kuthibiti teknolojia. Teknolojia haikudhibiti wewe. Unaweza kwa makusudi kuchagua kutumia teknolojia na vyombo vya habari kutimiza mema na kutafuta vitu ambavyo ni vya “uadilifu, vya kupendeza, au vyenye taarifa njema au vyenye kustahili sifa nzuri” (Makala ya Imani 1:13).

Bwana alisema, “Mimi, Bwana, nina kazi kubwa ya kufanywa na wewe” (Mafundisho na Maagano 112:6). Fikiria jinsi unavyoweza kutumia teknolojia ili kutimiza kazi ile kubwa na ubaki “ukijishughulisha kwa shauku katika kazi njema” (Mafundisho na Maagano 58:27). Unaweza kuhitaji kutumia teknolojia katika kazi yako. Unaweza kuitumia kupata aina zote za burudani. Inaweza kukusaidia uwasiliane na wengine. Na inaweza kukusaidia ujifunze, na ukue, na utimize kazi ya Bwana. Hata hivyo, matumizi mengine yanaweza kuwa yenye kuvuta mawazo, yasiyofaa, au yenye kudhuru. Kuliko kuruhusu teknolojia ikutawale wewe, tumia busara na mwongozo wa Roho ili kufanya maamuzi ambayo yanakuweka katika udhibiti.

2. Ninapotumia haki yangu ya kujiamulia kupanga mambo yajayo, ninahisi vizuri na kufanya chaguzi nzuri.

Pengine ulikuwa na uzoefu wakati ulipofanya uchaguzi kulingana na teknolojia ambayo haikuonekana kuwa sahihi. Inaweza kuwa ilihusisha vyombo vya habari ulivyotumia au muda uliotumika kwenye shughuli fulani. Badala ya kujawa na hofu kuhusu makosa uliyoyafanya, ni afya kufokasi juu ya ukuaji endelevu. Kama unapanga mambo yajayo, utafanya chaguzi nzuri zaidi kuliko kama unafanya maamuzi yote katika muda mfupi. Unaweza kuweka miongozo binafsi inayoenda sambamba na viwango vya injili ili ikusaidie ufanye chaguzi nzuri.

Kama unajikuta ukitumia vibaya au ukitumia vyombo vya habari kupitiliza, kuwa na ujasiri kujitahidi kubadilika. Kwa mfano, kama aina fulani za vyombo vya habari hazikuvutii au kuleta hisia nzuri, rekebisha tabia zako. Kama unatumia teknolojia kutumia vyombo vya habari au kujiingiza katika tabia unayojua siyo sahihi, kuwa na ujasiri wa kubadilika—na kuwa na subira kwako mwenyewe kadiri unapojitahidi kufanya mabadiliko hayo. Fikiria baadhi ya mambo ya utendaji unayoweza kufanya ili kubadilika. Kwa mfano, kama unaona vigumu zaidi kufanya maamuzi mazuri nyakati fulani za siku, unaweza kupanga nyakati utakazotumia teknolojia na nyakati ambazo hutatumia.

Vilevile, kama unatumia teknolojia kujiimarisha mwenyewe, kuunganika na wengine, na kutimiza kazi ya Bwana, na unamhisi Roho, endelea kufanya mambo hayo. Kwa vile wewe kwa hakika ni mwaminifu kuhusu chaguzi zako, imani yako katika Bwana inaweza kukusaidia utumie haki yako ya kujiamulia katika njia ambazo zinakuongoza uhisi vizuri na uendelee kufanya chaguzi bora.

3. Ninaweza kutumia haki ya kujiamulia ya uadilifu kutulia kidogo na kupumzika.

Unaweza kuhisi kwamba maswali kuhusu teknolojia na vyombo vya habari ni endelevu. Kiasi gani ni zaidi ya kawaida? Je, Ninapaswa kuongeza au kupunguza matumizi yangu ya vyombo vya habari na teknolojia? Je, ninatumia muda wangu kwa busara? Usijaribu kuacha mawazo kama haya yakushinde. Kumbuka kwamba ni SAWA kutulia na kupumzika kutoka kwenye vyombo vya habari. Kupumzika kunaweza kuwa kuchagua kufanya shughuli zingine badala ya kutazama skrini kwa masaa machache au hata kutotumia teknolojia fulani, kama vile mitandao ya kijamii, kwa kipindi kirefu.

Teknolojia inatoa baraka kubwa mno kutusaidia tubaki tumeunganika na wengine; hata hivyo, kwa sababu tu sisi tunaweza kuunganika wakati wowote haimaanishi tunahitaji kuwa tumeunganika wakati wowote. Bwana anatukumbusha, “Tulieni na jueni kuwa Mimi ni Mungu” (Mafundisho na Maagano 101:16). Hakikisha unatenga muda wa kuunganika Naye.

Iweni na Hekima

Wakati teknolojia inaendelea kukua, sisi sote tutakumbana na maamuzi mengi. Badala ya kuangalia Kanisani kwa ajili ya sheria na orodha mahususi, tunaweza kugeuka kwa Baba wa Mbinguni, Mwokozi, kwenye maandiko, na maneno ya manabii wa sasa kwa ajili ya kanuni za kusaidia kuongoza chaguzi zetu. Roho atatusaidia tujue kama chaguzi zetu ni sahihi. Maneno ya Yakobo yanatumika leo kama yalivyokuwa mwanzo wakati alipoyafundisha: “Ee iweni na hekima; niseme nini zaidi?” (Yakobo 6:12).