Liahona
Usajili wa Bila Malipo kwa Magazeti ya Kanisa Sasa Unapatikana
Machi 2024


“Usajili wa Bila Malipo kwa Magazeti ya Kanisa Sasa Unapatikana,” Liahona, Machi 2024.

Usajili wa Bila Malipo kwa Magazeti ya Kanisa Sasa Unapatikana

Picha
mwanamke akitazama gazeti

Magazeti ya Kanisa sasa yanapatikana kwa waumini ulimwengu kote bila malipo. Jiandikishe kwa ajili ya usajili wa mwaka mzima kwenye:

  • Liahona (kwa ajili ya watu wazima).

  • Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, (kwa umri wa miaka 12–18)

  • Rafiki (kwa ajili ya watoto)

Katika maelezo kuhusu mpango huu mpya, Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza , “Kanisa linataka kutoa fursa kubwa ya kuyafikia maneno ya manabii, na tunafurahi sana kufanya nakala zilizochapishwa za magazeti ya Kanisa zipatikane bila malipo“ (Aug. 1, 2023, news,ChurchofJesusChrist.org).

Jinsi ya Kujisajili ili kupata Magazeti Yaliyochapishwa

Toleo lako la kwanza litawasili ndani ya takribani miezi miwili.

Jinsi ya Kujiandikisha kwa ajili ya Ukumbusho wa Kila Mwezi wa Barua pepe

Kama ungependa kusoma magazeti ya Kanisa kidijitali, unaweza kujisajili ili kupokea taarifa ya barua pepe wakati toleo jipya linapopatikana kwenye tovuti ya Kanisa na katika app ya Maktaba ya Injili.