Liahona
Ninawezaje Kujumuisha Kitabu cha Mormoni katika Desturi Zangu za Pasaka?
Machi 2024


“Ninawezaje Kujumuisha Kitabu cha Mormoni katika Desturi Zangu za Pasaka?,” Liahona, Machi 2024.

Njoo, Unifuate

Pasaka

Ninawezaje Kujumuisha Kitabu cha Mormoni katika Desturi Zangu za Pasaka?

Picha
Yesu Anatokea katika Amerika

Yesu Anatokea katika Amerika, na Armold Friberg

Kitabu cha Mormoni kinatoa ushahidi wenye nguvu juu ya ukweli wa Bwana aliyefufuka, Yesu Kristo. “Sisi kama Watakatifu wa Siku za mwisho tumepewa zawadi kubwa mno ya Pasaka … kitabu cha Mormoni.”1

Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Sababu kubwa ya sisi kusherehekea Krismasi ni kwa sababu ya Pasaka.”2 Kwa namna sawa na jinsi baadhi ya familia wanavyosoma au kuigiza hadithi ya Krismasi kutoka Luka 2 wakati wa Krismasi, familia yako ingeweza kutumia shughuli zinazoambatana na kumsherehekea Mwokozi aliyefufuka katika Pasaka hii kwa kutumia 3 Nefi 11:1–17. Nyimbo zilizoorodheshwa zinahusiana na mistari iliyochaguliwa, lakini ungeweza pia kuchagua nyimbo zako za dini unazozipenda kuhusu Yesu Kristo.

Shughuli

Ukiwa na wanafamilia au wewe mwenyewe, soma na uimbe kuhusu Yesu Kristo akija kwa Wanefi baada ya Kufufuka Kwake.

Soma

Sikiliza au Imba

3 Nefi 11:1–7

This Is My Beloved Son,” mstari wa 2, Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 76.

3 Nefi 11:8–15

Did Jesus Really Live Again?,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64.

3 Nefi 11:16–17

Easter Hosanna,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69