Liahona
Nini Kilikuwa Kikiendelea Wakati wa Isaya?
Machi 2024


“Nini Kilikuwa Kikiendelea Wakati wa Isaya?,” Liahona, Machi, 2024.

Njoo, Unifuate

2 Nefi 11–19

Nini Kilikuwa Kikiendelea Wakati wa Isaya?

Picha
ramani ikionesha sehemu za wakati wa Isaya

Nefi alihisi kushawishika kushiriki mengi ya maneno ya nabii Isaya. Kuelewa mazingira ya kijiografia na kisiasa nyuma ya unabii wa Isaya inaweza kukusaidia uongeze ishara alizozitumia katika kutoa unabii kuhusu siku zake na zetu.

Ramani hii inaonesha falme katika siku ya Isaya. Unaweza kuitumia kufuatilia wakati Nefi akimnukuu Isaya. Isaya anaweza kuwa anataja sehemu katika njia mbalimbali: kwa jina lake, makao makuu ya mji, kabila kuu la Israeli, kiongozi wa kisiasa, au ishara zingine. Angalia tanbihi katika maandiko kwa ajili ya utambuzi zaidi.

1. Shamu

  • Makao makuu: Dameski

  • Iliisaidia Israeli kuishambulia Yuda kwa kutojiunga na ushirikiano dhidi ya Ashuru

  • Kiongozi: Rezini (ona 2 Nefi 17:1 4,8)

2. Israeli

  • Ufalme wa Kaskazini

  • Makao makuu: Samaria

  • Kabila kuu: Efraimu (ona 2 Nefi 17:8–9) au “makabila yaliyopotea”

  • Kiongozi: Peka, mwana wa Remalia (ona 2 Nefi 17:1 4,8)

3. Yuda

4. Ashuru

  • Uwezo wa kijeshi katika siku ya Isaya

  • Iliiteka Shamu, Israeli, na hatimaye eneo lote la Yuda isipokuwa Yerusalemu

  • Iliyatawanya yale makabila kumi

  • Baadaye ilitekwa na Babeli

  • Ishara ya kiburi na maangamizo ya waovu wakati wa Ujio wa Pili (ona 2 Nefi 20)

5. Babeli

  • Iliiteka Ashuru na Yuda

  • Iliwapeleka Wayahudi uhamishoni kutoka Yerusalemu

  • Ishara ya ulimwengu na uovu wake