Liahona
Ni Kwa Jinsi Gani Kuwa Mpatanishi Kunanisaidia Niikusanye Israeli?
Machi 2024


“Ni Kwa Jinsi Gani Kuwa Mpatanishi Kunanisaidia Niikusanye Israeli?,” Liahona, Machi 2024.

Njoo, Unifuate

2 Nefi 28

Ni Kwa Jinsi Gani Kuwa Mpatanishi Kunanisaidia Niikusanye Israeli?

Nefi aliona kwamba watu katika siku za mwisho wangegombana wao kwa wao (ona 2 Nefi 28:3–4, 20), lakini ugomvi siyo njia ya Bwana. Kwa kweli, kuikusanya israeli tunahitaji kuwa na “njia ya juu zaidi na takatifu zaidi”1 njia ya kuchangamana na wengine.

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Kama una nia ya dhati kuhusu kusaidia kuikusanya Israeli na kuhusu kujenga uhusiano ambao utadumu milele na milele, sasa ndio muda wa kuweka kando uchungu wote. Sasa ni muda wa kuacha kusisitiza kwamba ni kwa njia yako au la hakuna njia. Sasa ni muda wa kuacha kufanya vitu ambavyo huwafanya wengine wajizuie wakihofia kukukasirisha. Sasa ni muda wa kuzika silaha zako za vita. Kama ghala yako ya maneno imejaa matusi na mashitaka, sasa ni muda wa kuyatupilia mbali. Utainuka kama mwanamume au mwanamke wa Kristo aliye imara kiroho.”2

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawapenda watoto wote wa Mungu bila kujali tofauti zao. Shetani anajaribu kutumia tofauti zetu ili kutugawa lakini kwa kuchagua amani kuliko ugomvi, tunajenga mazingira ya kukaribisha ambayo yanawavuta watu kwenye injili ya Bwana iliyorejeshwa.

Fikiria hali zifuatazo na takafari njia unazoweza kujibu kwa upendo.

Picha
watu wakiwa wameinua juu ishara

Kama unahisi kuwa na hisia kali kuhusu mtazamo wa kisiasa, jinsi gani unaweza kuwa na uelewa mkubwa katika mazungumzo yako na wale ambao wana mtazamo unaopingana?

Picha
watu wawili wakiwa wamekaa na migongo yao ikiwa mkabala

Kama familia yako haielewani, ni jinsi gani unaweza kuleta mazingira ya amani yenye upendo na kukubalika kwao?

Picha
mwanamume mwenye hasira akiangalia kompyuta

Ikiwa unahisi kukasirishwa na kitu fulani unachosoma kwenye mitandao ya kijamii, ni kipi unaweza kufanya ili kuepuka kuingia kwenye mabishano?