Liahona
Kuongozwa Kwa usalama hadi Kule Tunakohitaji Kuwa
Machi 2024


“Kuongozwa Kwa usalama hadi Kule Tunakohitaji Kuwa,” Liahona, machi, 2024.

Njoo, Unifuate

2 Nefi 25-32

Kuongozwa Kwa usalama hadi Kule Tunakohitaji Kuwa

Mwokozi kwa uthabiti ataendelea kutusaidia kwenye safari yetu kwa njia za kipekee.

Picha
miguu ikitembea ndani ya theluji

Nilipokuwa na umri wa miaka 12, familia yangu ilihama kutoka karibu na sehemu ya tropiki ya Hong Kong kwenda sehemu yenye baridi, baridi ambalo sikulizoea. Punde, nilialikwa kwenye matembezi yangu marefu ya kwanza katika msimu wa baridi na vijana wakubwa katika kata yangu.

Siku ya matembezi yetu marefu, nilivaa vazi la kukinga baridi kadiri nilivyojua. Tulipokuwa tunapanda njia inayopindapinda mlimani, nilifurahi kuona theluji inayoanguka ikifunika ardhi. Nilikuwa sikuvaa vya kutosha kwa ajili ya mandhari na hali ya hewa, hata hivyo, na nilipata ugumu katika kwenda sambamba na kikundi changu. Niliwaambia waendelee na ningejiunga na wale ambao niliamini walikuwa nyuma yetu.

Nilipoendelea na mwendo wangu, viatu na nguo zangu zikawa zimelowa na mikono yangu, miguu, na uso vikafa ganzi. Na kisha theluji ilianza kudondoka kwa wingi sana kiasi kwamba sikuweza tena kuiona njia. Baada ya kutangatanga kwa muda fulani, nilitambua kwamba nilikuwa nimepotea, peke yangu, na pasipokuwa na uhakika kama mtu yoyote alijua kama nilikuwa nimepotea.

Wakati mwingine katika safari ya maisha, tutahisi kukosa maandalizi, tuliopotea, au tulioachwa nyuma. Tunaweza kupoteza hisia zetu za mwelekeo wa njia mbele yetu. Inaweza kuonekana kama kadiri tunavyojaribu kwa nguvu kubwa kusonga mbele, ndivyo tunavyokuwa mbali zaidi kutoka mwisho wa safari. Hali ya kuvunja moyo inaanza kuingia, na majaribu ya kukata tamaa yanakuwa ya kuvutia.

Kwa bahati nzuri, Mwokozi Yesu Kristo ana uwezo wa kuongoza hatua zetu, kutuinua wakati tunapojikwaa (ona Zaburi 37:23–24), na kutuleta kwenye pumziko (ona Mathayo 11:28), kuponywa (ona Isaya 53:5; Alma 15:8; Mafundisho na Maagano 42:48), kujiamini (ona Mafundisho na Maagano 121:45), na amani (ona Mosia 4:3; Alma 38:8; Mafundisho na Maagano 19:23). “Sogeeni karibu nami,” Alisema, “na mimi nitasogea karibu na nyinyi, nitafuteni kwa bidii nanyi mtanipata”(Mafundisho na Maagano 88:63). Njia ya haraka siku zote inaweza isiwe wazi, lakini tunaweza kumfuata Mwokozi kwa imani kwamba safari yetu itakwisha vizuri na kwa ushindi kwa sababu Yeye atatuongoza kwa usalama hadi kule tunakohitaji kuwa.

Daima tunaweza kutazama kwa Yesu Kristo kwa sababu Yesu Kristo ni “njia, kweli, na uzima” (Yohana 14:6).

Ni njia Sahihi kwa ajili ya Safari Yetu

Katika kujifunza kwetu Kitabu cha Mormoni mwaka huu, tumemfuata Lehi na familia yake kwenye safari yao kwenda nchi ya ahadi. Fikiria ni kitu gani familia ya Lehi ilivumilia wakati wa safari yao.

  • kudhihakiwa kwa ajili ya kuwaamini na kuwafuata manabii

  • kubadilishafaraja zilizozoeleka kwa nyika zisizojulikana

  • kusafiri bila kujua ni umbali kiasi gani, bila kujua mwisho wa safari, au muda wa safari

  • njaa, huzuni, ugonjwa, na kifo

  • kazi ngumu, wakati mwingine bila kuelewa sababu ya kazi hizo au jinsi ya kuzikamilisha

  • vipingamizi, ucheleweshaji, mfarakano, na kukatishwa tamaa

  • hali ngumu kwenye kulea familia changa

Njia mzima, pia tuliona jinsi Bwana kwa uthabiti alivyoendelea kuwasaidia. Alitoa

  • uongozi wa kinabii na ufunuo binafsi,

  • maandiko yaliyokuwa na baraka na maagano yaliyoahidiwa,

  • kumbukumbu ya nasaba na historia ya familia,

  • vifaa vipya na mbinu za kukidhi mahitaji yao,

  • ongezeko la uwezo wa kuvumilia shida,

  • hekima na maelekezo ya kukamilisha kazi zisizoeleweka,

  • Liahona (kifaa cha kuwasaidia kuongoza safari yao), na

  • usalama na ulinzi kwa ajili ya familia zao.

Kama familia ya Lehi safari zetu hazitakuwa bila changamoto na dhabihu. Mwokozi kadhalika atakuwa kwa unyoofu akiendelea kutusaidia katika njia zisizo na kifani. Nefi alifundisha, “Njia iliyo sawa ni kuamini katika Kristo … kwa uwezo wenu wote, akili, na nguvu, na nafsi zenu zote” (2 Nefi 25:29). Kama tunachagua imani katika Yesu Kristo, kwa unyenyekevu kupokea neno Lake, na kuwa na ujasiri wa kutenda, tutapata furaha na baraka katikati ya shida tunazokabiliana nazo. Njia nzima, tunaweza kuwa na ujasiri kwamba tunaweza kukamilisha kile anachokitaka sisi tukifanye (ona 1 Nefi 3:7).

Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo kupitia hizo Mwokozi anaendelea kutusaidia.

Picha
mchoro wa Yesu Kristo

Mapambazuko ya Siku Angavu, na Simon Dewey

Yeye Anatupa Sisi Mafundisho Yake

Yesu Kristo anajua “mwisho kutoka mwanzo” (Ibrahimu 2:8). Yeye pia “alitengeneza njia na kuongoza njia.”1 Mafundisho Yake, yanayojulikana katika maandiko kama mafundisho ya Kristo, ni njia ambayo sisi wote lazima tuifuate ili tukombolewe na kuokolewa.

Lazima tuendelee kuonesha imani katika Yesu Kristo, tutubu mara kwa mara, tubatizwe, tupokee kipawa cha Roho Mtakatifu, tuingie katika maagano, na tujaribu kwa uwezo wetu wote kuvumilia. Kama malipo, tunaahidiwa msamaha, tumaini, na uzima wa milele. (Ona 2 Nefi 31:2–20.)

Katika ulimwengu wa njia zinazotofautiana na njia zinazopingana, mafundisho ya Yesu Kristo yanatoa mwelekeo ulio wazi na wenye kutuekelezeka ambao tunaweza kuufuata ili kutufanya tuelekee kwenye njia sahihi (ona 2 Nefi 31:21).

Yeye Anatuletea Faraja

Kupitia dhabihu Yake ya kulipia dhambi, Mwokozi anajua hakika jinsi ilivyo kuwa mpweke na aliyesahaulika. Pia anajua kikamilifu jinsi ya kutuletea faraja. Yeye allisema, “Msifadhaike mioyoni mwenu” (John 14:1) na “sitawaacha ninyi yatima: naja kwenu” (John 14:18).

Mwokozi ameahidi zawadi ya Mfariji, ambaye ni Roho Mtakatifu, kwa wale wanaoamini katika Yeye. Yeye alisema kwamba Mfariji “atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha mambo yote” (Yohana 14:26).

Yeye Anatupatia Neno la Mungu

Kupitia Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika siku zetu, Bwana ametupa maandiko ya kale na maandiko ya siku za mwisho, ambayo yana neno la Mungu. Nefi alifundisha kwamba “yeyote atakayesikiliza hilo neno la Mungu, na alizingatie, … hataangamia” (1 Nefi 15:24).

Karamu ya kila siku ya neno la Mungu inaleta ulinzi na inatuongoza kupata uzoefu wa upendo wa Mungu kwa wingi zaidi. Neno lake linaangaza njia yetu (ona Zaburi 119:105) na “litatueleza [sisi] vitu vyote ambavyo [sisi] tunastaili kutenda”2 Nefi 32:3).

Yeye Anatuongoza kupitia Watumishi Wake—Manabii na Mitume

Yesu Kristo amewaita manabii na mitume ili watusaidie. Ushauri wao na mafundisho yao ni kwa ajili yetu na kwa ajili ya siku yetu. Ukijiona umepotea au umekanganyikiwa kwenye safari yako, inaweza kuwa ya kusaidia kutafakari maswali matatu yafuatayo:

  1. Ni kwa jinsi gani Bwana aliniandaa kupitia maneno ya manabii na mitume kwa ajili ya majaribu niliyoyapata?

  2. Ni kipi manabii na mitume wananialika nifanye leo ili kujiandaa kwa ajili ya changamoto ambazo zipo mbele?

  3. Ninafanya nini sasa ili kutenda juu ya mialiko ya kinabii?

Kwa kutafakari maswali haya, tunaweza kugundua umuhimu wa mwongozo wa manabii na mitume. Tunaweza kuisikia vyema sauti ya Bwana na kutambua jinsi Yeye kwa uendelevu anavyotusaidia. Kama tunachagua, tunaweza kuwasikiliza manabii na mitume na kupata mwongozo, ustawi, na ulinzi kwenye njia ambayo inaongoza kurudi kwa Baba wa Mbinguni na Mwanaye,Yesu Kristo.

Picha
Mzee Tai juu ya kilele cha mlima

Mzee Tai katika uwanja wa shabaha wa Sierra Nevada, California miaka ya 1988. Hadithi anayoshiriki ilitokea juu ya Mlima Baden Powell katika Milima ya San Gabriel ya California mnamo 1984.

Picha kwa hisani ya mtunzi

Imani ya Kusonga Mbele

Niliyepotea, mwenye baridi, na mpweke kwenye mlima ule wenye theluji miaka ile mingi iliyopita, nilikata tamaa. Bila kujua kitu kingine cha kufanya, nilipiga magoti katika theluji mpya iliyoanguka na nikasali kwa Baba yangu wa Mbinguni kwa ajili ya msaada. Nilishiriki hali yangu ngumu na woga pamoja Naye na nilisihi niweze kupatikana na kuokolewa

Nilipoinuka kutoka kwenye sala yangu, theluji ilianguka kunizunguka na uzuri, utulivu, ukimya uliijaza miti. Ushwari huu ulivurugwa wakati niliposikia sauti ya mchakariko katika vichaka karibu yangu. Vijana wawili wakubwa walitokea. Walikuwa tayari wamefika kileleni, na badala ya kufuata njia, waliamua kuteleza kushuka mlima. Katika sehemu zote, waliteleza moja kwa moja mpaka pale nilipokuwa!

Waliponiuliza nilikuwa nafanya nini pale, niliwaambia nilikuwa nimepotea. Walinialika nijiunge nao, na pamoja tuliteleza kwa usalama mpaka chini ya makutano ya njia chini ya mlima. Hatimaye tuliunganika na kundi letu lote.

Tunapokuwa tukienda mbele kwenye safari zetu binafsi kwa imani, moyo wa ibada, na uvumilivu, na tuweze kutambua jinsi Mwokozi anavyotembea pamoja nasi na kwa ukamilifu anatusaidia. Yesu Kristo ndiye njia, na kweli, na uzima. Imani yetu katika Yeye na iweze kuleta amani kwenye akili zetu na furaha kwenye safari yetu