Liahona
Ni Kipi Yesu Kristo Anaahidi Ambacho Ulimwengu Hauwezi?
Machi 2024


Ni Kipi Yesu Kristo Anaahidi Ambacho Ulimwengu Hauwezi?,” Liahona, Machi 2024.

Njoo, Unifuate

2 Nefi 20–25

Ni Kipi Yesu Kristo Anaahidi Ambacho Ulimwengu Hauwezi?

Picha
Upande wa kushoto, watu wanadhihaki na kuonesha kwa vidole; upande wa kulia, watu wakimsikiliza Yesu akifundisha

Maelezo ya kina kutoka Ndoto ya Lehi,, na Greg K Olsen; kielelezo cha Yesu akifundisha, na Justin Kunz

Ingawa maneno ya Isaya yanaweza kuwa magumu kueleweka, kitu kimoja ambacho ni wazi ni kwamba “Babeli … itakuwa kama wakati Mungu alipoipindua Sodoma na Gomora” (2 Nefi:23:19) na “waovu wataangamia” (ona 2 Nefi 23:22). Kwa nini mtu yeyote angechagua njia ya uovu?

Kuishi katika Babeli, au kuishi kwa uovu, kunaweza kuonekana kunavutia. Babeli inaweza kuahidi anasa za kiulimwengu, lakini injili ya Yesu Kristo inaahidi shangwe ya kweli na amani isiyo na mwisho.

Katika jedwali hili, fahamu tofauti kati ya jinsi ulimwengu unavyopendekeza kwamba tunapaswa kuishi na jinsi Yesu Kristo anavyotufundisha tuishi. Ni ahadi zipi ambazo ulimwengu unatoa kwa kufuata mafundisho yake ukilinganisha na ahadi Mwokozi anazoahidi kwa kufuata mafundisho Yake?

Ulimwengu unafundisha

Ahadi ya ulimwengu

Yesu Kristo anafundisha

Ahadi ya Yesu Kristo

Kuwa fidhuli na mwenye kiburi (2 Nefi 23:11)

Kuwa mnyenyekevu (3 Nefi 12:3)

Kuwa mwenye ufahari (2 Nefi 24:11)

Kuwa mpole (3 Nefi 12:5)

Kuwa mwenye hasira (2 Nefi 24:6)

Kuwa mpatanishi (3 Nefi 129, 22–24)

Tafuta utukufu wako mwenyewe (2 Nefi 24:13-14)

Tafuta utukufu wa Bwana (3 Nefi 12:16; 13:13, 33)

Hatutaangamia pamoja na waovu kama tunamfuata Yesu Kristo. Badala yake, tutaweza kuwa na uhakika kwamba Yesu Kristo “atakuwa mwenye huruma kwa watu [Wake]” (2 Nefi 23:22)