2021
Kusikia kuhusu Daraja Tatu za Utukufu kwa Mara ya Kwanza
Julai 2021


Njoo, Unifuate

Kusikia kuhusu Daraja Tatu za Utukufu kwa Mara ya Kwanza

Mafundisho na Maagano 76

Julai 5–11

Picha
artwork depicting the celestial kingdom

Kazi ya sanaa na Annie Henrie Nader

Sehemu ya 76 ya Mafundisho na Maagano inafafanua vipengele muhimu vya mpango wa wokovu ambavyo vilipotea kutoka duniani wakati wa ukengeufu. Kwa watu wengi, kujifunza kweli hizi zilizorejeshwa kwa mara ya kwanza ni uzoefu wa kukumbukwa. Hii ilikuwa kweli kwa Connie, mwongofu kutoka Richmond, Virginia, MAREKANI.

Anakumbuka: ”Siku zote nimeona upendo wa Mungu wakati ninaposoma Biblia, bali kamwe sikuweza kupata kanisa lolote ambalo lilifundisha kwa njia niliyoielewa. Wakati nilipopata somo la wamisionari juu ya mpango wa wokovu, nilijihisi kuthibitishiwa na amani kama ambavyo kabla sijaisikia kamwe. Nilijifikiria mwenyewe, ‘Huyo ni Baba wa Mbinguni ninayemjua.’ Kujifunza kuhusu madaraja ya utukufu kulifungua akili zangu kwa mapana sana kiasi kwamba sikuweza kuzuia msisimko wangu wa kujifunza zaidi.”

Delphine, mwongofu kutoka Paris, Ufaransa, ana hali ngumu ya kifamilia, kwa hiyo wakati wamisionari walipomfundisha kwamba familia zinaweza kuishi pamoja katika ufalme wa selestia, hakuwa na uhakika kama ni kitu anachokitaka. Wakati wamisionari walipoendelea kumfundisha kuhusu daraja tatu za utukufu, hata hivyo, alipata faraja. Alijifunza kwamba ataweza kuwa na wale anaowapenda waliochagua kuifuata injili. Pamoja na uelewa mzuri sana wa mpango wa wokovu, alisema, “niliona ni haki kabisa na hiyo ilinihakikishia.”

Picha
article on three degress of glory