2021
“Nitawaongoza”
Julai 2021


Njoo, Unifuate

Mafundisho na Maagano 77–80

“Nitawaongoza”

Ingawa tunaweza kuwa kama watoto kiroho, Bwana atatuongoza kama tunamwamini.

Picha
mission president meeting with missionary

Mmisionari alisema Roho alimnog’oneza kwamba ningemsaidia kupata jibu.

Vielelezo na David Malan

Katika Mafundisho na Maagano 78:17–18, Mwokozi anasema:

“Amini, amini, ninawaambia, ninyi ni watoto wadogo, nanyi bado hamjaelewa jinsi baraka kuu Baba alizonazo katika mikono yake mwenyewe na amezitayarisha kwa ajili yenu;

“Na hamwezi kustahimili mambo yote kwa sasa; hata hivyo, changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza. Ufalme ni wenu na baraka ni zenu na utajiri wa milele ni wenu.”

Kama vile kila mmoja wetu anavyofikiri kuhusu uzoefu wetu katika maisha, kwa hakika tutakumbuka nyakati ambapo Bwana alituongoza.

Imani ya Mmisionari

Nakumbuka wakati fulani ambapo Bwana aliwaongoza watu kadhaa. Nilikuwa nahudumia kama rais wa misheni katika Misheni ya Brazil Porto Alegre South. Mmoja wa wamisionari wetu alikuwa na tatizo la kupasuka taya la juu kwa ndani, ambalo halijawahi kutibiwa. Alipozungumza, hewa ilikwenda kupitia juu ya mdomo wake na kutokea puani mwake. Ilikuwa vigumu kwa wengine kumwelewa.

Mzee huyu kijana aliniambia kwamba ameomba kuhusu tatizo hili. Alisema Roho alimnong’oneza kwamba ningemsaidia kupata jibu. Imani yake ya kawaida, ya dhati ilinitia moyo. Nilimgeukia Mungu kwa ajili ya msaada katika kupata ufumbuzi.

Upasuaji mdogo ungeweza kusahihisha tatizo, bali kupata upasuaji haikuwa mchakato rahisi. Kama tungeufanya kibinafsi, ungekuwa ghali sana kwa familia ya mmisionari huyu. Kwa upande mwingine, kutumia mfumo wa huduma ya afya wa uma kungehitaji kuhudhuria mara kadhaa na kuna uwezekano wa kutumia miezi yote iliyobaki ya misheni yake.

Imani ya Mke wangu

Kila wakati ninapokuwa na kazi maalumu ya kukamilisha, ninategemea imani na msaada wa mke wangu. Nilielezea mtanziko wa mmisionari huyu kwake na kumwomba azungumze na watu wa hospitali ya serikali ya pale. Kulikuwa na njia yoyote upasuaji ungefanywa bila gharama na ndani ya muda uliobakia?

Baada ya kusali kwa ajili ya msaada, mke wangu alikwenda hospitalini. Alikumbana na foleni ndefu ya watu wanaosubiri kuzungumza na muuguzi. Wakati mstari uliposonga, mke wangu aliweza kusikia jinsi wagonjwa mbele yake walivyokuwa wanashughulikiwa. Hasa, watu waliambiwa kurudi kwa ajili ya matibabu mengine ndani ya miezi sita, wakati mwingie zaidi.

Mke wangu alijua hii itakuwa muda mrefu kwa mmisionari wetu. Alihisi msukumo wa kuondoka kutoka kwenye foleni na kwenda kwenye mlango mwingine. Kule alimpata mwajiriwa mwingine wa hospitali. Mke wangu alijitambulisha na akaelezea hitaji la mmisionari wetu.

Picha
a woman talking to a surgeon

Yule mwajiriwa alimwelekeza kuzungumza moja kwa moja na daktari mpasuaji, ambaye alikuwa hospitalini siku ile akifanya upasuaji kwenye ghorofa nyingine. Alielezea kwa daktari mpasuaji ni kitu gani wamisionari wanafanya na jinsi mmisionari huyu atabarikiwa kama angeweza kupata upasuaji kurekebisha kaakaa lake lililopasuka.

Daktari mpasuaji aliuliza baadhi ya maswali. Kisha alisema, “Tunaweza kupanga upasuaji ndani ya wiki mbili?” Alijaza fomu ya hospitali ambayo ilielezea upasuaji huu ulikuwa kwa manufaa ya jamii na kwamba alikuwa kibinafsi amevutiwa nao. Alimpa fomu msaidizi wake na alimwomba apange tarehe.

Siku kumi baadae, daktari mpasuaji alimfanyia upasuaji mmisionari wetu. Muda si mrefu mzee huyu alirudi kazini, kwa furaha na akizungumza kwa sauti safi. Kwa shauku mpya, alitambua kwamba Bwana amemwongoza.

Uzoefu wa mmisionari huyu ni ushuhuda kwamba Baba yetu anasikia maombi yetu na anatuongoza kwa mkono Wake.

Bila Mungu, Sisi Si Kitu

Ukizungumza kiroho, sisi ni kama watoto wadogo. Hatuelewi baraka kuu ambazo Baba wa Mbinguni ameziandaa kwa ajili yetu. Tunapokua kimwili, tunaanza kuelewa zaidi kuhusu sheria za kidunia ambazo zinatawala maisha yetu. Bali kamwe hatupaswi kuachia elimu ya kidunia kuwa muhimu zaidi kuliko kuelewa baraka kuu ambazo Baba wa Mbinguni ametuhifadhia.

Musa, nabii mkuu wa Agano la Kale, alipata uzoefu ambao ulimwonyesha jinsi alivyofahamu vitu kwa uchache. Baada ya “kuuona ulimwengu na miisho yake, na watoto wote wa binadamu ambao wako, na ambao waliumbwa; kwa hivyo alishangazwa na kustaajabu mno.” Kisha Mungu akaondoka. Musa aliachwa peke yake, na akaanguka chini.

“Na ikawa kwamba masaa mengi yalipita kabla ya Musa kurudiwa tena na nguvu zake za kiasili kama mwanadamu; naye alijisemea: Sasa, kwa jinsi hii ninajua kwamba mwanadamu si kitu, kitu ambacho sikukidhania” (Musa 1:8–10).

Kama Bwana aliweza kutuonesha vitu vyote ambavyo tungeweza kuvifanya kwa nguvu Zake, pengine tungeweza kuhisi kuzidiwa. Kama Musa, tungeweza kuona kwamba bila Mungu, sisi si kitu chochote.

Hatua kwa Hatua

Bali badala ya kuzidiwa, Bwana anatuongoza hatua kwa hatua. Hii inaturuhusu kufanikisha mengi zaidi kuliko ambavyo tungeweza sisi wenyewe.

“Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.

“Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu” (Isaya 55:8–9).

Kama Bwana asemavyo katika Mafundisho na Maagano 78:18, sisi “hatuwezi kubeba vitu vyote sasa.” Hatuwezi bado kuelewa kila kitu ambacho Anaelewa. Nini, basi, tunapaswa kufanya? Bwana anajibu: “Furahini!”

Kutembea kwenye njia ya agano kwa furaha kuu kunajumuisha kuwa mnyenyekevu, kama mtoto mdogo. Lazima tukubali kufundishwa na kuongozwa na Baba (ona Mafundisho na Maagano 112:10). Maisha ni magumu sana kiasi kwamba hatuwezi kiurahisi kudhibiti mambo yote ya safari yetu. Na hatuwezi kuelewa kila kimoja ambacho sisi, au wapendwa wetu, wanapitia hapa duniani.

Lakini tunapoamini katika Bwana na kumruhusu kutuongoza kwa mkono, tunaweza kukamilisha zaidi katika ufalme Wake kuliko ambavyo tungeweza kufikiria. Tutaweza zaidi kubariki maisha ya watoto wa Baba yetu wa Mbinguni. Tutaweza zaidi kutambua mkono wa Mwokozi katika maisha yetu. Tutaweza zaidi kuhisi shukrani kwa ajili ya huruma na upendo Wake usio na mwisho.

Baraka ni Zako

Hatimaye, Bwana anatuongoza kwa kutukumbusha kwamba “Ufalme ni wenu na baraka zake ni zenu na utajiri wa milele ni wenu” (Mafundisho na Maagano 78:18).

Ninarudi kwenye mfano wa mmisionari wangu. Aliongozwa kuomba msaada na alibarikiwa na upasuaji ambao sasa unamruhusu kuwasiliana kwa uwazi. Kisha aliongozwa kwa wale walio tayari kupokea injili na baraka zake, ikijumuisha ubatizo. Pia ninatazama mfano wa mke wangu. Ushuhuda wake ulikuwa wenye nguvu sana Bwana alipomwongoza. Kisha alifungua madirisha ya mbinguni na kuwamwaga baraka.

Nina shukrani nilifanya kazi pamoja na mmisionari huyu kijana, aliyejawa na imani yenye nguvu na ya kawaida. Na nina shukrani kwamba ninaweza kuishi milele na mke wangu, anayeweka mfano wa kumruhusu Bwana kumwongoza.

Kwa kweli ufalme na baraka ni zetu.