2021
Kubariki Mababu Zangu
Julai 2021


Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Kubariki Mababu Zangu

Nilipopokea baraka zangu za patriaki, moyo wangu ulijawa na upendo kwa ajili ya mababu zangu.

Picha
Abigahel Kinic holdidng up chart with family history information

Picha na Richard M. Romney

Nilizaliwa cameroon, nchi ya mababu zangu. Kisha nilihamia Ufaransa, ambapo niliishi, kusoma, na kufanya kazi kama nesi katika hospitali tofauti huko Paris. Sasa ninaishi Montreal, ambako bado nafanya kazi kama nesi.

Nimekuwa natafuta Kanisa la kweli la Yesu Kristo kwa miaka mingi. Nilipokutana na wamisionari Paris, Roho Mtakatifu alinishuhudia kwamba hatimaye nimekipata kile nilichokuwa nakitafuta—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Nilijawa na furaha nyingi kiasi kwamba nilifikiri lazima nitakuwa tayari nipo mbinguni! Nilidhamiria kuishi injli kwa ukamilifu.

Nilifundishwa kuwatafuta mababu zangu na kufanya ibada kwa niaba yao hekaluni. “Nilipopokea baraka yangu ya patriaki, niliambiwa kwamba nitakuwa mwokozi juu ya Mlima Sayuni na kuleta wokovu kwa familia yangu. Moyo wangu ukiwa umejawa na upendo kwa ajili yao; nisingeweza kuwaangusha. Tangu hapo, nimefanya kazi bila kuchoka kwenye historia ya familia na nasaba.

Siku zote nimejua kwamba nilizaliwa katika familia ya kifalme ya Cameroon, familia ya Bamoun. Simulizi za kimila na hadithi za kale zinasema kwamba watu hawa walitokea Assyria na kuchanganyika na watu wengine wakati wa uhamiaji wao. Wametunza uzao wao na waliandika historia yao tangu AD 1300. Nyaraka zipo katika maktaba ya kasri la kifalme. Miongoni mwa historia nyingi nyingine, zinaelezea hadithi ya babu wa baba yangu kutoka upande wa mama Fon-gouhouo, ambaye alitawala kutoka mwaka 1818 mpaka 1863.

Niliweza kurudi nchi yangu ya asili, na kama mmoja wa wanafamilia ya Bamoun, niliruhusiwa kuziona nyaraka hizi. Pia nilimtembelea mfalme, nilikutana na viongozi wengine wa serikali, na kuzungumza na wenye mamlaka kuhusu Kanisa na kuvutiwa kwake kwenye maswala ya historia ya familia. Nina shukrani kwamba, kupitia injili ya urejesho, ninaweza kuifanya sehemu yangu ya kubariki nchi yangu ya asili na mababu zangu.