2021
Kuushinda Upinzani
Julai 2021


Njoo, Unifuate

Kuushinda Upinzani

Mafundisho na Maagano 71–75

Juni 28–Julai 4

Picha
people gathered on a street corner with Church leader and missionaries

Kielelezo na Dan Burr

Ufunuo katika Mafundisho na Maagano 71 unamwelekeza Joseph Smith na Sidney Rigdon kwenda na kuhubiri katika juhudi za kupunguza hisia zisizo za urafiki ambazo zimejitokeza dhidi ya Kanisa kutokana na ukosoaji kutoka waumini ambao wamepoteza imani yao. Zaidi ya miaka 100 baadae, Mzee Spencer W. Kimball wa Akidi ya Mitume kumi na wawili alikuwa na uzoefu kama huo akihubiri kulilinda Kanisa.

Ziara ya Mzee Kimball huko Ecuador

Wakati wa ziara ya Otavalo, Ecuador, mnamo mwaka 1965, Mzee Kimball aliwaambia wamisionari kugawa Kitabu cha Mormoni kwa wenyeji wa Otavalan. Hata hivyo, wamisionari walikutana na upinzani wakati Waotavalan walipoanza kusambaza uongo kuhusu wao katika vijiji vya karibu, na wamisionari walipambana kuushinda uwongo.

Miaka miwili baadae, Mzee Kimball alijiunga na waumini wachache na wamisionari katika mkutano karibu na kituo cha basi cha pale. Wakati wenyeji walipoteremka kutoka kwenye mabasi, wamisionari waliwaalika kusikiliza kutoka kwa Mtume anayeishi wa Yesu Kristo. Punde tu, karibia watu 20 walikusanyika. Wakati wamisionari walipoanza mkutano wao, kundi lilikua kufikia zaidi ya 100.

Kisha Mzee Kimball akanena. Alieleza juu ya ujio wa Yesu Kristo katika nchi za Marekani. Alionesha mawinguni na alizungumza juu ya sauti tulivu, na ndogo kutoka mbinguni ambayo ilitangaza kujitokeza kwa Mwana wa Mungu, kama inavyopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Mzee Kimball alikumbuka, “Kila jicho lilifuata ishara yangu kwenye mbingu kama vile Mwokozi alikuwa pale akija kupitia mawingi mepesi.”1

Baada ya hili, wamisionari waliendelea kujaribu kuwafundisha Waotavalan. Wamisionari akina dada walimfundisha mwanaume aliyeitwa Rafael Tabango, ambaye alibatizwa mnamo Julai 14, 1968—mwenyeji wa kwanza Muotavalo Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Mke wake, Teresa, pia alijiunga na Kanisa. Chini ya miaka 15 baadae, kigingi kilianzishwa huko Otavalo, na Kaka Tabango aliitwa kama patriaki wa kwanza.

Picha
article on overcoming opposition

Muhtasari

  1. Shajara la Spencer W. Kimball, Mei 29, 1967, kama ilivyonukuliwa katika “Preaching in Peguche,” history.ChurchofJesusChrist.org/GlobalHistories.