2023
Nuru ya Ulimwengu
Januari 2023


“Nuru ya Ulimwengu,” Liahona, Jan. 2023.

Karibu kwenye Toleo Hili

Nuru ya Ulimwengu

Picha
mchoro wa Yesu Kristo

Maelezo kutoka Fokasi kwenye furaha, na Michael T. Malm

Tunaposafiri kupitia maisha haya ya duniani, tunakutana na majaribu, ikiwa ni pamoja na hali ngumu za kifamilia. Changamoto hizi zinaweza kutusababisha tujihisi tumetelekezwa, wenye wasiwasi au wenye mfadhaiko. Kama tukigeukia chanzo cha kweli cha nuru, Mwokozi Yesu Kristo, tutaweza kuzivuka vyema zaidi hali zetu ngumu.

Katika toleo hili, Rais M. Russell Ballard anaeleza kwa muhtasari njia tunazoweza kupita hadi kuyatatua matatizo yetu. Anasema, “nuru ya [Kristo] … inaondoa vivuli vya ulimwengu kutoka katikati yetu na akilini mwetu” (ukurasa wa 4).

Kama mtaalamu wa zamani wa masuala ya ndoa na familia, Nilifanya kazi na familia nyingi zilizokuwa zikikabiliana na majaribu ya kipekee. Familia ambazo zilitenga muda kila siku kumruhusu Kristo katika maisha yao zilipata wenzi wa nuru na upendo Wake wakati walipokuwa wakiyakabili mapambano yao. Ninashiriki baadhi ya hadithi hizo katika makala yangu kwenye ukurasa wa 8.

Nina shukrani kwa ajili ya fursa takatifu niliyokuwa nayo, kupitia kazi yangu, kuona familia na watu binafsi wakiungana na Mwokozi kwenye njia ya kuelekea kuwa watu wa Sayuni (ona Musa 7:18). Niliona kwa muda mfupi sehemu ndogo ya mbingu kila wakati nilipouona mkono wa Bwana katika maisha ya mtu fulani.

Kwa shukrani,

Christy Monson