2023
Jinsi Gani Ubatizo Unaonesha Utiifu?
Januari 2023


“Jinsi Gani Ubatizo Unaonesha Utiifu?,” Liahona, Jan. 2023.

Njoo, Unifuate

Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

Jinsi Gani Ubatizo Unaonesha Utiifu?

Mwokozi wetu ni mfano mkamilifu wa utiifu kwa Baba wa Mbinguni, alitamka, “Siyatafuti mapenzi yangu Mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka” (Yohana 5:30).

Mwokozi alibatizwa kuonesha utii kamili kwa Baba wa Mbinguni. Vivyo hivyo, wakati tunapoonesha utiifu wetu kwa kubatizwa, tunaingia kwenye agano na Mungu la kuwa wafuasi waliojitoa, watiifu wa Yesu Kristo. (Ona 2 Nefi 31:5–13.)

Picha
Yohana akimbatiza Yesu

Kielelezo kimoja cha utiifu wa Mwokozi kinapatikana katika hadithi ya ubatizo Wake.

“Wakati huo akaja Yesu kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana, ili abatizwe.

“Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?

“Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndiyo itupasavyo kuitimiza haki yote”.(Mathayo 3:13–15).

Yohana Akimbatiza Yesu, na Harry Anderson