2023
Familia Ni za Milele
Januari 2023


“Familia Ni za Milele,” Liahona,, Jan. 2023.

Misingi ya Injili

Familia Ni za Milele

Picha
familia ikitabasamu

Familia ni kitengo muhimu kwa jamii na kwa Kanisa. Waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaamini kwamba familia zinaweza kuwa za milele. Tunafanya kazi kuimarisha familia zetu duniani. Pia tunayo imani kwamba tunaweza kupata baraka ya familia ya milele.

Familia ya Mungu

Watu wote ni wana au mabinti wa kiroho wa wazazi wa mbinguni. Sisi sote ni sehemu ya familia ya Mungu. Sisi wote tuna asili ya kiungu na majaliwa. Kama tukiishi kwa haki, tunaweza kurudi kuishi na Baba yetu wa Mbinguni kama sehemu ya familia Yake milele.

Picha
wanandoa wapya wakiwa nje ya hekalu

Picha ya ndoa na Joseph Kaluba

Familia za Milele

Wakati mwanamume na mwanamke wanapokuwa wamefunga ndoa hekaluni na kuyashika maangano yao, ndoa yao itadumu milele. Ibada hii ya hekaluni inaitwa kuunganisha. Watoto watakaozaliwa baada ya wazazi wao kuunganishwa wanazaliwa ndani ya agano hilo. Watoto waliozaliwa kabla wazazi wao hawajaunganishwa wanaweza kuunganishwa nao ndani ya hekalu ili waweze kuwa familia milele. Waumini wa Kanisa wanafanya historia ya familia na kazi ya hekaluni ili waweze kuunganisha familia zao pamoja kupitia vizazi vyao vyote. Baraka ya familia ya milele inafanywa iwezekane kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Ndoa

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imeamriwa na Mungu. Injili ya Yesu Kristo inawafundisha waume na wake kuwa watiifu na kuaminiana wao kwa wao katika maagano yao ya ndoa. Wanapaswa kuwa wakweli katika mawazo, maneno na matendo. Ndoa ni ubia ulio sawa na wanandoa wanapaswa kutiana moyo, kufarijiana na kusaidiana.

Picha
wazazi wakiwa na mtoto mchanga

Wazazi na Watoto

Mungu aliwaamuru Adamu na Hawa kuwa na watoto. Viongozi wa Kanisa wamefundisha kwamba amri hii bado ina nguvu. Akina mama na akina baba wanafanya kazi pamoja ya kuwalea watoto wao kwa upendo na uadilifu (ona Mafundisho na Maagano 68:25–28). Watoto wanafundishwa kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao (ona Kutoka 20:12).

Kufundisha na Kujifunza

Wazazi wanawafundisha watoto wao kumpenda Mungu na kutii amri Zake. Maisha ya familia yanatupa sisi nafasi za kuhisi furaha na kujifunza subira na kuacha ubinafsi. Tabia hizi zinatusaidia kuwa zaidi kama Mungu na kutuandaa kuishi kwa furaha kama familia milele.

Kuimarisha Familia

Inahitaji kazi, kujitolea kwa dhati na subira ili kujenga familia yenye mafanikio. Kanuni za injili kama vile imani, sala, msamaha, upendo, kazi na burudani yenye kuleta siha vinaweza kutusaidia kupata shangwe katika maisha ya familia. Tunaweza pia kupata ufunuo binafsi kujua jinsi ya kuimarisha familia zetu.

Picha
mchoro wa Yesu Kristo

Picha ya Kristo, na Heinrich Hofmann

Baraka Zinapatikana kwa Wote

Sio kila mtu anayo fursa kuwa sehemu ya familia iliyo bora hapa duniani. Lakini Mungu ameahidi kwamba kila mtu anayetii amri Zake atapokea baraka zote za famila ya milele. Tunaweza kumtumainia Yeye na kuwa na imani katika wakati Wake.