2023
Wakati Ugonjwa wa Kudumu Unapokujia
Januari 2023


Wakati Ugonjwa wa Kudumu Unapokujia,” Liahona, Jan. 2023.

Kuzeeka kwa Uaminifu

Wakati Ugonjwa wa Kudumu Unapokujia

Kushughulika na shida za siku hadi siku kunaweza kutusaidia kukua katika huruma, uwezo wa kuhisi anachopitia mwingine na uthabiti.

Picha
mkono mmoja wa mtu ukishikilia mkono wa mtu mwingine

Kabla hajafariki kutokana na ugonjwa wa kudhoofisha, mama yangu mara kwa mara alitabasamu na kusema, “Hakuna kati yetu watakaotoka hapa duniani wakiwa wazima, kwa hiyo tunapaswa kufanya vyema zaidi kwa kile tulichonacho.”

Hiyo ilikuwa kwenye siku zake njema. Na katika maisha yake, alikuwa na siku zake njema nyingi.

Lakini pia alikuwa na siku ambazo hazikuwa za kuchangamsha sana. Kwenye siku hizo yeye angesema, “Chukua kile kinachokuja kwako na ona kama bado unaweza kufanya kitu kidogo kizuri ulimwenguni.”

Ulimwenguni, watu wanaishi muda mrefu zaidi sasa kuliko siku zilizopita.1 Lakini ingawa tunaishi muda mrefu, pia tunaelekea zaidi kuwa na magonjwa ya kudumu: kisukari, kutetemeka na kukakamaa, saratani, mfadhaiko, kufa kwa seli za ubongo, na orodha inaendelea. Kwa hiyo, wakati ugonjwa wa kudumu unapokujia, jinsi gani unapaswa kujibu?

Songa Mbele kwa Imani

“Kabili muziki, hata wakati ambapo huwezi kuimba tuni yake,” anasema kaka aliyelazimishwa kukubali likizo ya ulemavu wakati mke wake akirejea kufanya kazi ili kuisaidia famila yao. Anaamini kwamba mara nyingi tunakuwa na sura ya furaha ambayo inatuzuia kuchakata hisia zetu au kuboresha mwonekano wetu wa nje. “Badala ya kusonga mbele kwa imani, tunabaki palepale tukisubiri muujiza au kulalamika pale muujiza usipokuja,” anasema. Anavumilia kwa kusikiliza maandiko na mazungumzo ya mkutano mkuu na kuzungumza na marafiki na familia kwenye simu.

“Ni ukawaida wa kila siku ndio unaoweza kunishusha chini,” anasema dada ambaye mumewe ni mgonjwa wa kudumu. “Afya ya mume wangu kamwe haitatengemaa. Ninalikubali hilo. Lakini ugumu wa ratiba yote, majukumu madogo madogo yanachosha kiakili, kimwili na kiroho.” Anafurahia matembezi kutoka kwa akina dada wahudumu. “Wanapokuwa wamekuja kwa kweli huichangamsha siku yangu.”

“Wakati mwingine, mimi na mke wangu tunasahau mambo na tunakasirikiana,” anasema kaka mwingine anayeelekea uzeeni. “Tunahisi kukasirika tunapokuwa wasahaulifu mno na hususan majuto baada ya kuwa tumetoleana maneno ya hasira.” Wamejifunza kuandika muhtasari ili kuwasaidia kukumbuka. Wanapeana muda kwa kila mmoja kutulia kabla ya kuzungumza. “Na,” anasema, “tumejifunza hata zaidi umuhimu wa kusema, ‘Asante sana,’ na ‘nakupenda.”

Wanandoa wengine wazee waliishi kwa kipato kidogo kilichopangiliwa hadi pale bei za dawa zao zilipoongezeka mara mbili zaidi. Shukrani kwa wanafamilia na kata yao, mahitaji yao yalishughulikiwa. “Hapo mwanzo tuliona aibu kuomba msaada, hususan kutoka kwa watoto wetu,” yule kaka alisema. “Lakini kila mmoja alikuwa tayari kusaidia.”

Picha
Yesu anamponya mtu

Maelezo ya kina kutoka Aliwaponya Wengi wenye Magonjwa ya Kila Aina, na J. Kirk Richards, isinakiliwe

Mapendekezo na maoni

Hapa kuna baadhi ya mapendekezo na maoni kutoka kwa wale ambao wanashughulika na magonjwa ya kudumu:

  1. Wale wanaomgeukia Mwokozi watapata tumaini. Nilifikiri hamna yoyote ambaye angeweza kuelewa kile nilichokuwa napitia,” anasema kaka mwenye dalili za ugonjwa wa uchovu (CFS). “Ndipo Jumapili moja wakati nikishiriki sakramenti, nilitambua Mwokozi alielewa mateso yangu. Nilijua ningeweza kuvumilia kwa kumkaribia Yeye.” (Ona Alma 7:11–12, Mafundisho na Maagano 121:8, 122:8.)

  2. Huruma inaongezeka kwa wale ambao “wanastahimili vyema.” (Mafundisho na Maagano 121:8). “Tunamtazama nani, katika siku za huzuni na maafa, kwa ajili ya msaada na faraja? … Ni wanaume na wanawake walioteseka, na kutokana na uzoefu wao katika kuteseka wanaleta mbele utajiri wa huruma yao na rambirambi kama baraka kwa wale wenye uhitaji sasa. Je, wangeweza kufanya hivi kama wao wenyewe wasingeteseka?”2

  3. Chukua siku moja kwa wakati mmoja. “Miaka mingi iliyopita, maumivu yalikuwa makali sana sikujua jinsi ambavyo ningeweza kuvumilia zaidi. Nilianza kufikiria kujiua,” alisema dada anayeugua ugonjwa wa kukatika mawasiliano kati ya ubongo na uti wa mgongo (MS). Alijipeleka mwenyewe kwenye kitengo cha afya ya akili hospitalini. Wakati wa ushauri, dhima yake ikawa siyo tu “vumilia mpaka mwisho” (1 Nefi 22:31) bali “vumilia mpaka mwisho wa siku.”

  4. Kuza shauku mpya na zitafute njia mpya za kuhudumu. Badala ya kusikitika juu ya nini huwezi tena kufanya, gundua shauku mpya. Dada mwenye MS aligundua asingeweza kufanya mambo aliyoyapenda hapo mwanzo, kama kupanda na kuendesha farasi au softball. Badala yake, alijifunza kaligrafia. Sasa anatumia kipaji chake kipya alichokigundua kutengeneza miswada yenye rangi za kumetameta ya Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya familia yake.

Wakati ugonjwa wa kudumu unapokuwa ukweli wa maisha, unakuwa changamoto hasa. Lakini kwa imani, tumaini katika Kristo na tamaa ya kuendelea kuhudumu kushughulika na shida za siku hadi siku kunaweza kutusaidia kukua katika huruma, uwezo wa kuhisi anachopitia mwingine na uthabiti.

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Muhtasari

  1. Ona Susanne Reiff, “Kuongeza Matarajio ya Muda wa Kuishi: Watu wanazeeka na kuzeeka,” Alumniportal Deutschland, Sept. 2017.Alumniportal deutschland.org/en/global‑goals/sdg‑03‑health/increasing‑life‑expectancy‑age‑ageing.

  2. Orson F. Whitney, “A Lesson from the Book of Job” Improvement Era, Nov. 1918, 7.