2023
Auckland, New Zealand
Januari 2023


“Auckland, New Zealand,” Liahona,, Jan. 2023.

Kanisa Liko Hapa

Auckland, New Zealand

Picha
ramani ya ulimwengu ikiwa na duara kuzunguka New Zealand
Picha
mandhari ya Auckland, New Zealand

Picha kutoka Getty Images

Aukland ni mji wenye eneo lenye watu wengi mno nchini. Mwongofu wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho nchini New Zealand alibatizwa mnamo mwaka 1854. Leo, Kanisa katika nchi ya New Zealand lina:

  • Waumini 116,900 (kwa makadirio)

  • Vigingi 30, kata na matawi 229, misheni 3

  • Hekalu 1 linakarabatiwa huko Hamilton, 1 linajengwa huko Auckland

Picha
familia ikitembea nje

Mambo yote Yanashuhudia

Fabian na Adrienne Kehoe na binti yao wanafurahia maisha kwenye shamba katika bonde la Maromaku. “Tuna shukrani kwa neema ya nchi hii,” Adrienne anasema. “Na mambo haya yote yanashuhudia juu ya muumbaji mwenye upendo.”

Zaidi kuhusu Kanisa New Zealand

Picha
mama na binti

Mama na binti huko New Zealand wanashiriki muda wa upendo pamoja.

Picha
familia mezani

Baba na mwana wanajiunga na familia yao kwa ajili ya usiku wa wiki ya kujifunza Njoo, Unifuate.

Picha
Hekalu la Hamilton New Zealand

Hekalu la Hamilton New Zealand, kwa sasa likiwa kwenye ukarabati, liliwekwa wakfu mwaka 1958. Hekalu lingine linajengwa huko Auckland.

Picha
Watoto wakiangalia magazeti

Watoto huko New Zealand, kama vile watoto ulimwenguni kote, wanafurahia kusoma gazeti la Rafiki.

Picha
Familia na kondoo

Mama na baba wanawafundisha watoto wao jinsi ya kuwalisha kondoo. Leo huko New Zealand, kuna karibia kondoo watano kwa kila mtu, kushuka kutoka kilele cha ishirini na mbili kwa kila mmoja mwaka 1982.

Picha
wavulana

Wenye ukuhani wa Haruni wanajifunza injili pamoja wakati wa mkutano wao wa akidi.

Picha
wanaume wakicheza ragbi ufukweni

Ragbi na ufukwe ni maarufu kote nchini New Zealand.