2023
Mwaliko wa Mwokozi wa Kushiriki Nuru Yake
Julai 2023


“Mwaliko wa Mwokozi wa Kushiriki Nuru Yake,” Liahona, Julai 2023.

Karibu kwenye Toleo Hili

Mwaliko wa Mwokozi wa Kushiriki Nuru Yake

Picha
Yesu na wanafunzi wakiwa njiani kuelekea Emau

Njiani Kuelekea Emau, na Wendy B. Keller, courtesy of Havenlight

Kabla hajapaa kwenda mbinguni, Kristo aliyefufuka aliwaalika Mitume Wake wa Agano Jipya kuwa mashahidi Wake “hata mwisho wa nchi.” (Matendo ya Mitume 1:8). Wakiwa wametiwa moyo na jukumu hili, Mitume “hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo” (Matendo ya Mitume 5:42).

Katika makala yake katika toleo hili, Mtume wa siku za leo, Mzee Quentin L. Cook, anaelezea jinsi tunavyoweza kushiriki injili ya Mwokozi licha ya mapungufu yetu. Anaandika, “Tunapoishi injili, kuwapenda na kuwatumikia wengine, tukisimama imara dhidi ya majaribu na mateso, na kutoa ushuhuda kwa maneno na matendo, tutawaleta wengine kwa Yesu Kristo” (ukurasa wa 4).

Kwa sisi wenyewe kusogea karibu na Mwokozi, tutakuwa tunafundisha kupitia ushuhuda na mfano. Atakuwa miongoni mwetu, kama nilivyoelezea katika makala yangu kwenye toleo hili, kama tutaheshimu maagano yetu na kutafuta ushauri Wake kupitia maneno ya manabii (ona ukurasa wa 40).

Katika kujifunza kwetu kuhusu huduma ya Mitume kwenye Njoo, Unifuate ya mwezi huu, na tutafakari jukumu letu wenyewe na wito wetu wa kushiriki nuru ya Mwokozi na wale wanaotuzunguka. Kristo alipaa kwenda mbinguni kitambo sana, lakini tunapomwomba Yeye “kukaa pamoja nasi” (Luka 24:29) leo, Yeye atatembea pamoja nasi hatua kwa hatua.

Mzee Patricio M. Giuffra

Wa Sabini