2023
Je, Unaamini katika Mungu?
Julai 2023


“Je, Unaamini katika Mungu?,” Liahona, Julai 2023.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Je, Unaamini katika Mungu?

Rafiki yangu aliposhiriki dukuduku yake, nilipokea uelewa wa ghafla.

Picha
msichana na mvulana wakiongea pamoja

Kielelezo na Katy Dockrill

Nikiwa nakua, sikuwahi kutilia shaka ukweli wa injili. Nilipofikia miaka ya ujana, hata hivyo, nilijihoji kama kweli nina ushuhuda au nilikubali tu kile ambacho wazazi wangu na marafiki walikiamini. Niliomba usiku huo ili kwamba nijue kwamba injili ni ya kweli.

Licha ya masumbuko yangu, msichana niliyekutana naye katika chuo changu cha umma aliniambia alihisi kwamba naelewa lengo langu na uelekeo katika maisha.

“Je, unaamini katika Mungu?” aliniuliza.

Nilimjibu ndiyo na kwamba kanisa langu hufundisha uhusiano wetu pamoja na Mungu na lengo la maisha. Pia nilimwambia kuhusu Nabii Joseph Smith na Urejesho. Alisikiliza kwa makini.

Jumapili iliyofuata kanisani, nilibeba vijitabu kuhusu Joseph Smith na mpango wa wokovu kwa ajili ya rafiki yangu. Baada ya kuvisoma na kuanza kusoma Kitabu cha Mormoni, nilienda naye kanisani.

Baadaye aliniambia amekuwa karibu sana na kaka yake mkubwa. Alikuwa amekuwa ni rubani wa maonyesho ya ndege ya eneo lake. Kwa huzuni, katika majira ya joto kabla hatujakutana, aliuawa akiwa anaendesha ndege kwenye maonyesho. Alihuzunishwa sana na kifo chake na alikuwa na dukuduku kumhusu kwa sababu alijdai kutoamini katika Mungu. Alikuwa ameomba ili kujua hali yake na msimamo ulikuwaje mbele za Mungu.

Aliposhiriki dukuduku yake, nilipokea uelewa wa ghafla. Ilikuwa ni hisia ya ukweli halisi na nuru. Nilitambua kwamba kukutana kwetu hakukuwa kwa bahati tu. Bali, Mungu alisikia na kujibu ombi la dhati la msichana huyu aliyevunjika moyo.

Nilinyenyekezwa kujua kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa ananijua na angeniona ninayefaa kuwa nyenzo katika mikono Yake katika kujibu ombi la msichana yule. Nilielewa hekima Yake kuu katika kutumia uzoefu huu kujibu pia ombi langu la kujua kwamba injili ni ya kweli.

Baada ya kujiandaa, nilipakia mabegi yangu kwa ajili ya miaka miwili bora ya maisha yangu. Wakati huo, rafiki yangu alifundishwa na wamisionari pamoja na dada yake. Wote wawili walijiunga na Kanisa na hatimaye kutumikia misheni. Baada ya misheni yangu, rafiki yangu aliniomba nifanye ibada za hekaluni kwa ajili ya kaka yake.

Najua kwamba Mungu husikia na kujibu maombi ya dhati, ingawa wakati mwingine katika hali au muda tusiotarajia.