2023
Misukumo ndani ya Hekalu
Julai 2023


“Misukumo ndani ya Hekalu,” Liahona, Julai 2023.

Misukumo ndani ya Hekalu

Nyumba ya Bwana ni nyumba ya ufunuo. Tunapokwenda hekaluni mara kwa mara, ndivyo tunavyopokea ufunuo wetu kwa wingi.

Picha
Hekalu la Houston Texas

Picha ya Hekalu la Houston Texas Hekalu na Steve Scott Jackson

Nyumba ya Bwana sio tu ni jengo takatifu ambapo tunafanya kazi za wokovu lakini pia ni sehemu ya ufunuo, ambako misukumo mikubwa na midogo huweza kuja, ambako majeraha kwenye nafsi zetu yanaweza kuponywa na ambako Bwana anaweza kuchochea mioyo yetu katika njia zisizotarajiwa.

Msukumo wa tofauti

Nilipokuwa nikihudumu kama mfanyakazi wa maagano katika Hekalu la Houston Texas, kundi la waendesha pikipiki walifika na kuuliza kama wanaweza kuingia hekaluni. Rais wa hekalu, Richard Sutton, alilielezea kundi lile lengo la hekalu na hitaji la kibali cha hekalu ili kuingia ndani ya jengo. Kiongozi wa waendeshaji hao pamoja na mwenza wake walikuwa makini sana.

“Nilihisi kitu tulipopita karibu na jengo lenu,” alisema. “Siwezi kukielezea, lakini ilikuwa ni msukumo wa tofauti kwamba nilihitaji kujua ni nini kiliusababisha.”

Wenza wale walihitaji kujua zaidi, hivyo Rais Sutton aliandaa wamisionari kwenda kumtembelea.

Zaidi ya mwaka na nusu baadaye , Rais Sutton alisikia hodi kwenye mlango wa ofisi yake hekaluni. “Hutanitambua, lakini kitambo kilichopita nilifika hapa na baadhi ya marafiki kwenye pikipiki zetu. Kwa kipindi hicho, niliweza kuangalia tu kutokea nje.” Akiwa ameshikilia kibali cha hekalu, “Leo nitaangalia kutokea ndani.”

Picha
mwanamke akitembea nje ya hekalu

Lugha ya Pili

Wakati Dean na Bonnie Hill walipoitwa kutumikia kama wamisionari wazee huko Hekalu la Cochabamba Bolivia, Bonnie alikuwa mwenye hofu. Hakuwahi kujifunza Kihispania na alikuwa na mashaka kuhusu uwezo wake wa kufanya ibada stahiki au kujumuika na wenzake katika lugha asiyoijua. Baraka ya ukuhani ilimhakikishia kwamba angeweza kuwasiliana kwa sauti na kiroho katika Kihispania.

“Siwezi kuzungumza Kihispania sana nje ya hekalu,” anasema. “Lakini ndani ya nyumba ya Bwana, inaonekana inakuwa vyepesi kwangu.”

Hata baada ya yeye na mume wake kurejea nyumbani na kuhudhuria vikao kwa Kihispania katika Hekalu la Ogden Utah, wahudumu walishangaa lafudhi yake maridadi.

Fanya Kitu Upate Shangwe

Rais Russell M. Nelson alisema, “Tunaweza kupewa mwongozo wa kiungu siku nzima kuhusu uzoefu wa hekaluni na historia ya familia ambao wengine wamepata. Lakini tunatakiwa kufanya kitu fulani ili tuweze kuipata furaha hiyo sisi wenyewe.”1

Shangwe na mwongozo wa kiungu pamoja na misukumo na hakikisho vinatusubiria ndani ya hekalu. Huko kuna lugha ya kimbingu ikiongelewa na kueleweka huko ambayo haipatikani kwingine kokote duniani. Tunapata ufunuo ambao Bwana anatamani kutupatia ndani ya hekalu pale ambapo si tu tunahudhuria hekalu lakini pia tunakwenda huko tukitarajia kupokea ufunuo. Hapa ni baadhi ya mifano ya miongozo ya kiungu iliyopokelewa:

  • Martin Goury wa Cote d’Ivoire alitafuta mwongozo hekaluni katika suala la muhimu la maisha na alikuwa na uthibitisho maridadi kwamba maombi yake yamejibiwa kuhusu kitu hicho. Hii ni kanuni ambayo Bwana alimfundisha Oliver Cowdery: “Rejesha mawazo yako juu ya usiku ule uliponililia katika moyo wako. … Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili?” (Mafundisho na Maagano 6:22, 23).

  • Randy Bronson anaishi karibu na Hekalu la Payson Utah na ametumia miaka mingi kufanya utafiti wa historia ya familia. “Lakini nilikuwa na mtoto asiyehudhuria kikamilifu, na sikujua jinsi ya kufanya kwa ajili yake. Kwa hiyo sikuweka tu jina lake kwenye orodha ya maombi, lakini nilisali kwa dhati hekaluni, nikijaribu kujua nini cha kufanya kumhusu. Napata hisia ya jinsi ya kusema au kufanya kwa ajili yake.”

  • “Wewe ni mama mwema,” Stephanie Fackrell Hill alisema kwa mtu asiyemfahamu katika Hekalu la Logan Utah. “Unajuaje?” mama yule kijana aliuliza kwa kusita. Dada Hill alisema, “Niliona mchoro wa watoto wako kwenye mikono yako, na nilipoiona, nilivuviwa na Roho kukwambia.” Mama yule kijana alikuwa akijaribu kuficha mikono yake. Sasa alihisi kukubalika na sio wa kutiliwa shaka.

Hekalu sio tu sehemu ya kusaidia kuwaokoa wafu wetu lakini pia kupokea aina ya ufunuo ambao unaweza kutuongoza sisi na watu wengine kwenye njia ya agano. Rais Nelson alisema, “Kila mmoja wetu anahitaji kuimarishwa kiroho kunakoendelea na kufundishwa ambako kunawezekana tu katika nyumba ya Bwana.”2 Misukumo hii na uvuvio vinavyopokelewa ndani ya nyumba Yake takatifu hutufundisha kuona kama Yesu aonavyo, kusikia kama asikiavyo na kuishi kama aishivyo. 

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Mihutasari

  1. Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Kufungua Mbingu kupitia Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia,” Liahona, Okt. 2017, 19.

  2. Russell M. Nelson, “Kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Liahona, Nov. 2018, 114.