2023
Kuishi na Kushiriki Injili
Julai 2023


“Kuishi na Kushiriki Injili,” Liahona, Julai 2023.

Kwa ajili ya Wazazi

Kuishi na Kushiriki Injili

Picha
wasichana wakiangalia maandiko pamoja

Wapendwa Wazazi,

Njia mbili tunazomwonyesha Mungu shukrani zetu kwa ajili ya injili ni kwa kuiishi na kuishiriki. Makala katika toleo la mwezi huu yamefokasi kwenye kuifanya injili ya Yesu Kristo sehemu kubwa ya maisha yetu, iwe kupitia kuimarisha imani Kwake, kufanya marekebsho ya msingi au kutangaza kweli Zake ulimwenguni kote. Shangwe huwasubiria wale wanaojifunza na kufuata mafundisho ya Mwokozi na kushiriki ujumbe Wake kwa maneno na vitendo.

Mijadala ya Injili

Kushiriki Injili kupitia Ushuhuda

Alika kila mwanafamilia kushiriki ushuhuda mfupi kutoka kwenye kanuni pendwa ya injili. Shiriki nukuu kuhusu kazi ya umisionari kutoka kwenye makala ya Mzee Quentin L. Cook iliyopo ukurasa wa 4. Ukifikiria kanuni ya injili uliyoishiriki, uliza: Je, kuna watu ambao tunaweza kushiriki nao kanuni hizi?

Hisi Kuwa Karibu Zaidi na Yesu Kristo

Waulize watoto wako wakati wanapohisi kuwa karibu zaidi na Yesu Kristo. Tengeneza orodha iliyo na majibu yao. Elezea kuhusu shughuli tano za kujenga imani za Mzee Patricio M. Giuffra (ona kurasa za 42–43). Kama familia, fikirieni kufanya mojawapo ya shughuli hizi ambayo mnakubaliana nayo kwamba italeta tofauti nyumbani mwenu. Weka mpango wa pamoja wa kufokasi kwenye shughuli hiyo kwa mwezi huu.

Badiliko Linaweza Kupelekea Ukuaji wa Kiroho.

Badiliko, linalotarajiwa na lisilotarajiwa, ni sehemu ya uzoefu wetu katika maisha ya duniani. Soma makala ya Mzee Ciro Schmeil iliyopo ukurasa wa 30 kuhusu aina tofauti za mabadiliko katika maisha yetu. Je, ni kwa jinsi gani mabadiliko haya yanaweza kutusaidia kuwa zaidi kama Mwokozi?

Njoo, Unifuate Burudani ya Familia

Mungu Anawapenda Watoto Wake Wote

Matendo ya Mitume 10

“Mungu hana upendeleo: bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na Yeye” (Matendo ya Mitume 10:34–35).

Viongozi Wakuu wenye Mamlaka hutokea nchi mbalimbali. Karibia nusu yake hutokea Marekani. Wengine hutokea Amerika ya Kati na Kusini, Asia, Ulaya, Africa, Oceania, Mexico na Kanada.

  • Je, unaweza kumtaja Mtume aliyezaliwa Ulaya?

  • Unaweza kumtaja Mtume kutokea Amerika ya Kusini?

  • Unaweza kumtaja Mtume ambaye wazazi wake walitokea Swideni na Ufini?

  • Unaweza kumtaja Mtume ambaye familia yake ni chimbuko kutokea China?

Tunaweza kutokea sehemu tofauti, lakini Mungu anatupenda sote.

Mjadala: Ni katika njia gani tunaweza kuwa sawa au wa tofauti na watu wengine? Je, Mungu anatupenda kwa kuzingatia vile tunavyoonekana au kule tunakotokea? Rejelea hadithi ya Petro na Kornelio iliyopo katika Matendo ya Mitume 10. Walijifunza nini kuhusu kuwahukumu wengine? Tabia zipi ni za muhimu kwa Bwana?